in

Hizi Hapa Simu za Tecno za Bei Rahisi Zaidi Mwaka Huu (2020)

Simu hizi bei zake zina anzia kati ya Tsh 250,000 hadi Tsh 300,000

Simu za Tecno za Bei rahisi

Simu za Tecno ni moja kati ya simu zinazotumiwa na watu wengi sana hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla, Simu hizi zimekuwa zikitumiwa na watu wengi kwa sababu ya unafuu wake wa bei na hivyo kurahisisha mawasiliano miongoni mwa watumiaji wengi wa simu hizi.

Kuliona hili leo Tanzania Tech tunakuletea list ya simu za Tecno za bei rahisi, ikiwa pamoja na sifa za simu hizo pamoja na sehemu unazoweza kununua simu hizo kwenye maduka mbalimbali au kupitia mitandao mbalimbali. Vilevile kwenye list hii tutaenda kuangalia simu za tecno za bei rahisi ambazo ni kati ya shilingi za kitanzania Tsh 250,000 hadi Tsh 300,000. Basi bila kupoteza muda twende tukaangalie list hii ya simu hizi za bei nafuu.

1. TECNO L8 Lite

Simu ya Tecno L8 Lite ni moja kati ya simu za tecno za bei rahisi, simu hii inakuja na sifa za kawaida huku ikiwa na uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa battery yake yenye uwezo wa 4,000mAh, sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno L8 Lite

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 2
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0 Marshmallow
 • Uwezo wa Battery – 4000mAh Li-Ion
 • BEI – 200,000 – 250,000

NUNUA HAPA KWA TSH 220,000

2. TECNO  F2

Tecno F2 ni moja kati ya simu ambazo pia ni simu za bei nafuu kutoka kampuni ya Tecno, simu hii imezinduliwa hivi karibuni na inakuja na mfumo wa Android Nougat pamoja na sifa nyingine kama zifuatazo.

Sifa za Tecno F2

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 8
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 2
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
 • Uwezo wa Battery – 2000mAh Li-Ion
 • BEI – 150,000 – 250,000

NUNUA HAPA KWA TSH 169,000

3. TECNO Pop 1

Tecno Pop 1 ni simu ya bei nafuu ya tecno ambayo nayo pia ilizinduliwa sambamba na simu ya Tecno F2, Simu hii inakuja na kioo kikubwa na ni moja kati ya simu nzuri na za bei nafuu kutoka kampuni ya Tecno.

Video : Ugumu na Ubora wa Simu Mpya ya iPhone 12 Pro

Sifa za Tecno Pop 1

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya qHD IPS Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 8
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 2
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
 • Uwezo wa Battery – 2500mAh Li-Ion
 • BEI – 190,000 – 250,000

NUNUA HAPA KWA TSH 197,000

4. TECNO Spark K7

Simu nyingine ya Bei nafuu kutoka Tecno ni simu ya Tecno Spark K7, simu hii ni nzuri sana kwa umbo lake na pia ni moja kati ya simu zenye kamera nzuri kutoka na yenye uwezo wa kudumu na chaji. Sifa nyingine za Tecno Spark K7 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Spark K7

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya qHD IPS Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 8
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 5
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
 • Uwezo wa Battery – 3000mAh Li-Ion
 • BEI – 200,000 – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 224,000

5. TECNO WX4

Simu nyingine ya bei rahisi ni Tecno WX4, simu hii ya tecno inakuja na kioo kikubwa cha inch 5.0 pamoja na uwezo mzuri wa battery. Sifa nyingine za Tecno WX4 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno WX4

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya HD IPS Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 8
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
 • Uwezo wa Battery – 2800mAh Li-Ion
 • BEI – 290,000 – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 255,000

6. TECNO WX3

Tecno wx3 pia ni simu nyingine ya bei nafuu kutoka kampuni ya Tecno. Simu hii inakuja na uwezo wa kawaida na ni simu nzuri sana kwa wale wanaotaka kwenda na bajeti. Sifa za Tecno Wx3 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno WX3

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 8
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 5
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 5
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
 • Uwezo wa Battery – 2300mAh Li-Ion
 • BEI – 250,000 – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 250,000

7. TECNO R6

Simu ya Tecno R6 ni moja kati ya simu zinazojulikana sana hapa Tanzania, mbali na kujulikana simu hii pia ni ya bei nafuu sana na inakuja na sifa zifuatazo.

Sifa za Tecno R6

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 8
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 2
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 5
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 6.0 Mashmalow
 • Uwezo wa Battery – 2300mAh Li-Ion
 • BEI – 150,000 – 300,000
TECNO Spark 4 Kupata Android 10 na HiOS 6.2.0

NUNUA HAPA KWA TSH 195,000

8. TECNO Spark 2

Simu nyingine ya tecno ya bei rahisi ni Tecno spark 2, simu hii imezinduliwa hivi karibuni na inakuja na uwezo mzuri wa kamera pamoja na kioo kikubwa bila kusahau mfumo wa Android Go. Sifa nyingine za Tecno spark 2 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Spark 2

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 8
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo GO Edition
 • Uwezo wa Battery – 3500mAh Li-Ion
 • BEI – 250,000 – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 280,000

9. TECNO Spark K8

Tecno spark k8 ni simu ya bei nafuu sana kutoka kampuni ya Tecno, simu hii inakuja na muundo muzri lakini mbali na hayo simu hii inakuja na uwezo wa mtandao wa 4G pamoja na kamera nzuri na battery inayodumu na chaji zaidi. Sifa nyingine za Tecno Spark K8 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Spark K8

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya IPS Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 5
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
 • Uwezo wa Battery – 3000mAh Li-Ion
 • BEI – 290,000 – 300,000

NUNUA HAPA KWA TSH 270,000

10. TECNO Spark 3 (3G)

Hizi Hapa Simu za Tecno za Bei Rahisi Zaidi Mwaka Huu (2020)

Tecno spark 3 ni simu nzuri na ya bei nafuu kutoka kampuni ya Tecno, simu hii imezinduliwa hivi karibuni na inakuja na sifa bora na nzuri sana. Mbali na hayo simu hii imeboreshwa sana upande wa kamera kwani inakuja na kamera zenye mfumo wa AI pamoja na uwezo mkubwa wa kupiga picha hasa wakati wa usiku, sifa za tecno spark 3 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Spark 3

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya IPS LCD Capacitive Touchscreen
 • Ukubwa wa Ndani – GB 16
 • Ukubwa wa RAM – GB 2
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 8
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 na Megapixel 2
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 Pie
 • Uwezo wa Battery – 3500mAh Li-po
 • BEI – 290,000 – 300,000

Na hizo ndio simu za tecno za bei rahisi kwa sasa, unaweza kupata simu hizi kupitia maduka mbalimbali ya Tecno hapa Tanzania. Pia unaweza kupata simu nyingine za nzuri za tecno zenye kamera nzuri kwa kusoma makala hii hapa. Kama unahisi kuna simu yoyote ya tecno ya bei rahisi tuliyo isahau kwenye list hii unaweza kutuandikia kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

7 Comments

 1. Hakika Simu ni zuri na bei yake ipo vizuri tu tatizo linakuja unapo kwenda dukani kununua unakuta bei tofauti na hii iliyoandikwa mtandaoni inakuwaje? Pili mbona Simu hizi za Tecno zinastak Mara kwa Mara nini tatizo ?