Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A21s

Fahamu hizi hapa sifa kamili za simu mpya ya Samsung Galaxy A21s
Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A21s Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A21s

Kampuni ya Samsung hivi leo imetangaza ingizo jipya la simu mpya ya Galaxy A21s, simu ambayo ni toleo la maboresho la simu za Galaxy A20 ya mwaka jana 2019 na Galaxy A21 iliyotoka mapema mwaka huu 2020.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A21s

Simu hii mpya ya Galaxy A21s, inakuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na muonekano mpya wa kamera, pamoja na uwezo wa battery ambayo sasa inakuja na uwezo zaidi. Tukiangalia simu hii inakuja na kioo chenye ukubwa wa inch 6.5, kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED huku ikiwa na uwezo wa kuonyesha picha na video zenye resolution ya hadi pixel 720 kwa 1600.

Advertisement

Kwa juu simu hii inakuja na kamera iliyopo juu ya kioo ambayo inakuja na uwezo wa hadi Megapixel 13, kamera hii inao uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p. Kwa upande wa kamera za nyuma, Galaxy A21s inakuja na kamera nne ambapo kamera kuu inakuja na uwezo wa Megapixel 48 na kamera nyingine tatu zinakuja na uwezo wa Megapixel 8 na nyingine mbili za mwisho zikiwa na Megapixel 2 kila moja. Kamera zote kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua video za hadi pixel 1080p@30fps.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A21s

Kwa upande wa sifa za ndani, Galaxy A21s inakuja na processor ya Exynos 850 yenye speed ya CPU ya hadi Octa-core (4×2.0 GHz & 4×2.0 GHz). CPU hiyo inasaidiwa na RAM ya hadi GB 6, huku kukiwa na matoleo mengine yenye GB 3 na GB 4. Kwa upande wa uhifadhi wa ndani, Galaxy A21s inakuja na ROM ya GB 32 huku ikiwa na toleo lingine lenye GB 64.

Simu hii inakuja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint iliyopo kwa nyuma ya simu hiyo pamoja na sensor nyingine kama vile accelerometer, na proximity. Galaxy A21s inakuja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, hadi sasa bado haijathibitshwa kama simu hii inakuja na Radio FM ila uwezekano wa simu hiyo kuwa na Radio ni mkubwa.

Kwa upande wa battery Galaxy A21s inakuja na battery ya Li-Po yenye uwezo wa 5000 mAh battery. Kama kawaida ya simu nyingi za samsung, simu hii pia inakuja na teknolojia ya Fast Charging ambayo huwezesha simu hii kujaa chaji kwa haraka.

Kama unataka kujua bei ya simu hii unaweza kusoma Hapa Kujua Bei kamili pamoja na sifa za undani za simu hii mpya ya Galaxy A21s kwa Hapa Tanzania.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use