Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A51

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya Samsung Galaxy A51
Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A51 Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A51

Hatimaye baada ya tetesi za muda mrefu, hivi leo kampuni ya Samsung imezindua rasmi simu zake mpya za daraja la kati zitakazo tarajiwa kuanza mwaka 2020. Galaxy A51 na Galaxy A71 ni simu mpya kabisa kutoka Samsung zilizo zinduliwa siku ya leo tarehe 12/12/2019 huko nchini Vietnam.

Tukianza na Galaxy A51, simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.5 kilicho tengenezwa kwa teknojia ya Infinity-O Super AMOLED display, kioo ambacho pia kinakuja na resolution ya FullHD+. Juu ya kioo hicho kuna kamera ya sefie ya Megapixel 32, pamoja na sehemu ya Fingerprint ambayo inapatikana chini ya kioo.

Advertisement

Kwa nyuma Galaxy A51 inakuja na mtindo mpya wa kamera ambao haujawahi kutumiwa na kampuni ya Samsung, mtindo huo umebeba kamera nne ambazo zinakuja na uwezo wa Megapixel 48 kwa kamera kuu, Megapixel 12, pamoja na Megapixel 5 kwa kamera nyingine mbili zilizobakia. Kamera hizo zinakuja na sehemu mbalimbali kama vile Smart Switch, Live Focus, na Super Steady Video, huku ikiwa na uwezo wa kurekodi video hadi za 1080p@30fps.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A51

Kwa upande wa sifa za ndani, Galaxy A51 inaendeshwa na processor ya Exynos 9611 yenye speed ya CPU hadi Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53). Processor hii inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani wa GB 128, uhifadhi huu unaweza kuongezwa kwa kutumia MicroSD Card yenye uwezo wa hadi TB 1.

Kwa upande wa battery simu hii inaendeshwa na battery yenye uwezo wa 4,000 mAh, huku ikiwa na uwezo wa kudumua na chaji hadi siku moja nzima bila kuchaji kabisa kutokana na matumizi yako. Vilevile simu hii inakuja na teknolojia ya Fast battery charging ya hadi W15 hii ikiwa na maana unaweza kupata asilimia 50 ya chaji kwa muda wa dakika 20 tu.

Bei ya Samsung Galaxy A51

Kwa upande wa bei ya Galaxy A51, simu hii inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia desemba 16, huku kwa mujibu wa Samsung simu hiyo ikitarajiwa kuuzwa kwa Vietnamese dong VND7,990,000 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania TZS 805,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika. Soma hapa kuona sifa kamili za Samsung Galaxy A51.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use