Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A71

Kampuni ya Samsung imezindua simu mpya ya Samsung Galaxy A71
Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A71 Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A71

Hapo juzi kampuni ya Samsung ilizindua simu za aina mbili huko nchini Vietnam, Galaxy A51 ambayo najua tayari unajua sifa zake, pamoja na Galaxy A71 ambayo ningependa uhifahamu leo. Ingawa Galaxy A51 na Galaxy A71 zinafanana kwa muonekano, lakini kwa upande wa sifa simu hizi zina utofauti kidogo, hasa kwa upande wa bei, kamera, ukubwa wa kioo pamoja na sifa nyingine za ndani.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A71

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, Galaxy A71 inafanana sana na Galaxy A51 lakini tofauti yake kubwa ni kioo ambacho kwenye simu hii kimeongezwa ukubwa kidogo hadi inch 6.7. Kioo hicho kimetengenezwa kwa teknolojia hiyo hiyo kama Galaxy A51.

Advertisement

Kingine cha utofauti kwenye simu hii ni pamoja na kamera za nyumba ambazo zinakuja na uwezo mkubwa zaidi ya A51, Simu hii inakuja na kamera nne kwa nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 64 badala ya 48 ambayo ipo kwenye Galaxy A51. Kamera nyingine zinakuja na Megapixel sawa na A51 yani Megapixel 12 huku nyingine mbili zikiwa na Megapixel 5 kila moja.

Tofauti nyingine ya simu hii na A51 ni RAM, Galaxy A71 inakuja na machaguo mawili yaani simu yenye RAM ya GB 6 na simu yenye RAM ya GB 8, pia vilevile simu hii inakuja na processor ya tofauti na A51 ambapo hii inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 730 ambayo inakuja na speed ya CPU ya hadi Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 470 Gold & 6×1.8 GHz Kryo 470 Silver).

Mbali na hayo Galaxy A71 pia inakuja na battery kubwa zaidi ya 4500 mAh battery uku ikiwa na teknolojia ya kuchaji battery kwa haraka ya Fast Charging ya Watt 25, hii ikiwa na uwezo wa kujaza simu yako chaji hadi asilimia 50 kwa muda wa dakika 30. Unaweza kusoma hapa kuona tofauti ya Galaxy A71 na Galaxy A51.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A71

Bei ya Samsung Galaxy A71

Kwa upande wa bei pia simu hizi zinatofautina kwa mujibu wa Gadgetsnow, Galaxy A71 inategemea kuanza kupatikana kuanzia mwezi wa kwanza na bei yake inatarajiwa kuwa shilingi za kitanzania TZS 1,200,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kupanda au kushuka kwenye masoko mbalimbali.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use