Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Huawei Kuzindua Simu Mpya ya Huawei Y6 (2019) Nairobi

Hizi hapa ndio sifa pamoja na bei ya Huawei Y6 (2019)
Huawei Kuzindua Simu Mpya ya Huawei Y6 (2019) Nairobi Huawei Kuzindua Simu Mpya ya Huawei Y6 (2019) Nairobi

Kampuni ya Huawei kupitia tawi lake la Nairobi nchini Kenya, hivi karibuni inatara kuzindua simu mpya ya Huawei Y6 (2019). Simu hii inakuja ikiwa inafanana kabisa na simu mpya ya Huawei Y6 Pro (2019) ambayo nayo ilizinduliwa hivi karibuni.

Simu hii mpya ya Huawei Y6 (2019), inakuja na kioo cha inch 6.09 chenye resolution ya 720 x 1560 pixels ambacho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD. Simu hii inakuja na kamera moja kwa mbele yenye Megapixel 8, huku kwa nyuma ikiwa inakuja na kamera moja ambayo ina Megapixel 13.

Advertisement

Huawei Kuzindua Simu Mpya ya Huawei Y6 (2019) Nairobi

Kama nilivyo kwambia simu hii haina tofauti sana kwa upande wa sifa na Huawei Y6 Pro (2019), kwani kuanzia muundo hadi sifa, simu hizi zote zinafanana. Tofauti kubwa iliyopo kwenye simu hizi ni uwezo wa RAM kwani Huawei Y6 (2019) inakuja na RAM ya GB 2, wakati Huawei Y6 Pro (2019) inakuja na RAM ya GB 3. Pia kitu kingine ni fingerprint ambayo inapatikana kwenye Huawei Y6 (2019) na haipo kwenye Huawei Y6 Pro (2019).

Sifa za Huawei Y6 (2019)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.09 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa EMUI 9
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6761 Helio A22 (12 nm).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – RAM GB 2.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye LED Flash na uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye f/1.8, PDAF. Huku ikisaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3020 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, microUSB 2.0.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Midnight Black, Sapphire Blue.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Accelerometer, proximity.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma)

Bei ya Huawei Y6 (2019)

Kwa upande wa bei, Huawei Y6 (2019) inatarajiwa kuingia sokoni ikiwa inauzwa takribani euro 150, ambayo ni sawa na takribani Tsh 395,000 bila kodi. Kwa nchini Nairobi simu hii inategemewa kuuzwa kwa Kshs 17,999.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use