Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Nova 4e

Hizi hapa sifa kamili pamoja na bei ya Huawei Nova 4e
Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Nova 4e Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Nova 4e

Kampuni ya Huawei hivi leo imetangaza kuja na simu mpya ya Huawei Nova 4e, simu hii mpya kutoka kampuni ya Huawei inasemekana kuwa itakuja kwenye nchi nyingine ikiwa kwa jina la Huawei P30 Lite.

Kwa sasa simu hizi mpya za Huawei P30 na P30 Pro, zinatarajiwa kutoka hivi karibuni huku simu hii ikiwa kama ndio simu ya bei rahisi kutoka kampuni hii. Anyway kwa upande wa Huawei Nova 4e inakuja na sifa nzuri sana huku ikiwa imejikita zaidi kwenye kamera kama zilivyo simu nyingi za Huawei.

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Nova 4e

Advertisement

Simu hii inakuja na kioo cha inch 6.15 chenye resolution ya 1080 x 2312 pixels pamoja na teknolojia ya IPS LCD. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Megapixel 32 yenye uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps, kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu za Megapixel 24, 8 pamoja Megapixel 2, huku kamera zote zikisaidiwa na Flash ya LED Flash.

Simu hii inaendeshwa na processor ya Kirin 710 SoC ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 au GB 6, huku ikisaidiwa na ukubwa wa ndani wa GB 128. Huawei Nova 4e inakuja na battery ya Li-Po 3340 mAh yenye teknolojia ya Fast charging, Sifa nyingine za Huawei Nova 4e ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei Nova 4e

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.15 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2312 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Hisilicon Kirin 710 (12 nm).
 • Uwezo wa GPU – Mali-G51 MP4.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 128.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 yenye f/2.0, HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 24 yenye f/1.8, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 ambayo ni 13mm (ultrawide) na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2 ambayo ni f/2.4, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3340 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0 Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Midnight Black, Pearl White na Gradient Blue.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Huawei Nova 4e

Kwa upande wa bei, Huawei Nova 4e inakuja rasmi sokoni nchini China kuanzia March 21 na inatarajiwa kuuzwa kwa Yuan CNY 1,999 ambayo ni sawa na Tsh 697,000 kwa simu yenye RAM GB 3, na toleo lenye RAM ya GB 6 litauzwa kwa Yuan CNY 2,299 ambayo ni sawa na Tsh 802,000. Kumbuka bei hizi ni bila kodi hivyo bei inaweza kuongezeka kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use