Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J8

Hili ndilo Toleo bora la Simu za Galaxy J Series kwa sasa
Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J8 Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J8

Najua ulikua unadhani tumemaliza na simu za Samsung kwa siku ya leo, lakini kuna simu moja kutoka Samsung ambayo ningependa uifahamu, Simu hiyo ni Samsung Galaxy J8, Simu hii imezinduliwa leo huko nchini India pamoja na simu mpya za Galaxy J4 pamoja na Galaxy J6.

Tofauti na simu zote za J Series zilizo zinduliwa leo Galaxy J8 ni simu nzuri zaidi ambayo inakuja na sifa nzuri pamoja na muonekano wa kisasa zaidi. Galaxy J8 inakuja na Kioo cha inch 6 chenye teknolojia ya Super AMOLED chenye resolution ya 720p. Simu hii inaendeshwa na processor ya Snapdragon 450 chipset huku ikisaidiwa na RAM ya GB 4. Vilevile simu hii inakuja na kamera mbili kwa nyuma.

Sifa za Samsung Galaxy J8 (2018)

Advertisement

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1480 pixels, 18.5:9 ratio (~274 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53, Qualcomm SDM450 Snapdragon 450 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – GB 4
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye f/1.9, LED flash
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/1.7,) na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye (f/1.9), autofocus, pamoja na LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold na Blue
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), Face Detection (Kufungua kwa Kutambua Uso).

Bei ya Samsung Galaxy J8

Kwa upande wa bei ya Galaxy J8, bado haijajulikana rasmi ila kama uko nchini india utaweza kununua simu hii kuanzia tarehe 20 mwezi ujao na utaweza kupata kwa kupunguzo ukinunua simu hii kupitia soko la mtandaoni la Flipkart la nchini india.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use