BlackBerry Kuja na Simu Mpya ya BlackBerry KEY2 Mwezi Ujao

Baada ya BlackBerry KeyOne sasa ni BlackBerry KEY2
BlackBerry KEY2 BlackBerry KEY2

Japokuwa simu za BlackBerry hazina watumiaji wengi lakini bado kampuni hiyo haijakata tamaa na inaendelea na utengenezaji wa simu mpya. Hivi karibuni kampuni hiyo ya nchini marekani imetangaza ujio wa simu mpya ya BlackBerry KEY2, toleo jipya la simu ya mwaka jana la Blackberry KeyOne.

Kwa mwaka huu 2018, Simu hiyo inaonekana kuja na kamera mbili kwa nyuma, flash ya LED flash pamoja na keyboard yenye vibonyezo vilivyo zoeleka kwenye simu za BlackBerry, simu hiyo pia inasemekana kuja na programu za messenger apps, BlackBerry Hub, Privacy Shade, pamoja na kibonyezo kipya cha app drawer shortcut.

Advertisement

Japo kuwa simu ya mwaka jana ya BlackBerry KeyOne haikufanya vizuri kwa kuuza nakala chache, takriban nakala 850,000 duniani kote, lakini bado kampuni hiyo ina matumaini ya kufanya vizuri kwa kuja na simu hii mpya ambayo kama ulivyo ona kwenye video hapo juu inategemea kuzinduliwa rasmi mwezi ujao tarehe 7 mwaka huu 2018.

Kwa habari zaidi za kuhusu simu hiyo mpya ya BlackBerry Key2 pamoja na sifa na bei yake kwa hapa Tanzania, endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza yote kuhusu simu hiyo mpya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use