Kampuni ya Honor Yazindua Simu Mpya ya Honor V20

Hizi hapa ndio sifa pamoja na bei ya simu mpya ya Honor V20
Kampuni ya Honor Yazindua Simu Mpya ya Honor V20 Kampuni ya Honor Yazindua Simu Mpya ya Honor V20

Baada ya kuripotiwa kuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 26 hatimaye kampuni ya Honor apo jana imezindua simu mpya ya Honor V20 au Honor View 20. Simu hii inakuja kama simu ya mwisho kwa mwaka 2018 kutoka kampuni ya Honor, Kampuni ambayo ni sehemu ya kampuni ya Huawei kutoka nchini China.

Kitu kikubwa kwenye simu hii mpya ya Honor View 20 ni kamera iliyotengenezwa na kampuni ya Sony yenye Megapixel 48 ambayo pia inakuja na Sensor mbili za 3D ToF sensor. Kwa mbele simu hii inakuja na kioo cha Inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya LCD ambacho pia kina resolution ya 1080 x 2310 pixels. Kama ilivyo simu mpya ya Galaxy A8s na Simu mpya ya Galaxy S10, Simu hii inakuja na kamera ya mbele ambayo iko juu ya kioo.

Kamera Honor V20

Advertisement

Kamera hiyo ya Selfie inakuja na uwezo wa Megapixel 25 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps. Simu hii inatumia processor kutoka kampuni ya Huawei ya Kirin 980, ambayo inasaidiwa na RAM ya kati ya GB 6 na GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128 au GB 256.

Honor V20

Kwa upande mwingine Honor View 20 inakuja na teknolojia ya AI kwenye kamera zake, Battery kubwa ya 4,000 mAh ambayo pia inakuja na teknolojia ya Fast Charging yenye uwezo wa kuchaji simu hiyo hadi asilimia 55 kwa muda wa dakika 30. Sifa nyingine za Honor View 20 au Honor V20 ni kama zifuatazo.

Sifa za Honor View 20 (Honor V20)

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.4 chenye teknolojia ya IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resoluti ya 1080 x 2310 pixels (~398 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.6 GHz Cortex-A76 & 2×1.92 GHz Cortex-A76 & 4×1.8 GHz Cortex-A55.
 • Aina ya Processor – Hisilicon Kirin 980 (10 nm)
 • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP10
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja ina GB 128 na nyingine ikiwa na GB 256 zote zenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja yenye RAM ya GB 8 na nyingine ikiwa na GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 25 yenye (f/2.0, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko tatu moja ikiwa na Megapixel 48 (f/1.8 PDAF), Nyingine zikiwa na sensor za TOF 3D stereo camera na  zote zinasaidiwa na Flash ya LED Flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 4000 mAh yenye teknolojia ya Fast battery charging 5V/4.5A 22.5W.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Sea Blue, Red na Magic Night Black.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Honor View 20

Kwa upande wa bei Honor View 20 inatarajiwa kuuzwa kwa Yuan ya China CNY2,999  ambayo ni sawa na Tsh 1,005,000 kwa toleo lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 128, Toleo lenye GB 128 na RAM ya GB 8 yenyewe itauzwa kwa Yuan CNY3,499 ambayo ni sawa na Tsh 1,173,000. Toleo la mwisho lenye RAM ya GB 8 na ukubwa wa ndani wa GB 256 itauzwa kwa Yuan CNY3,999 ambayo ni sawa na Tsh 1,340,000, kumbuka bei zote hizo ni bila kodi hivyo kwa Tanzania au Kenya bei hii inaweza kuongezeka kutokana na kodi na viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use