Sasa Unaweza Kupakua Toleo Jipya la iOS 9.3

Sasa Unaweza Kupakua Toleo Jipya la iOS 9.3 Sasa Unaweza Kupakua Toleo Jipya la iOS 9.3

Sasa watumiaji wa vifaa vya Apple yani iPhone, iPad, AppleTV na iPod wanaweza kupata toleo jipya la iOS 9 yani iOS 9.3 moja kwa moja kutoka katika vifaa vyao. Toleo hilo jipya la iOS lilianza kupakuliwa rasmi na watu mbalimbali duniani kuanzia tarehe 21 March 2016 ikiwa ni sambamba na siku ya uzinduzi wa vifaa vipya vya Apple yaliyofanyika huko Cupertino, California. Bofya hapa kuangalia tukio zima jinsi lilivyokua

Kama unataka kujua kama umeshapata toleo hilo jipya kwenye kifaa chako fuata maelekezo haya, nenda kwenye settings, general alafu software update hapo utaweza kupakua na ku-intall toleo hilo jipya la iOS 9.3 katika kifaa chako.

Haya ni baadhi ya mambo yaliyo ongezwa kwenye toleo hilo jipya la iOS  yani iOS 9.3, kumbuka kupata toleo hili ni bure kabisa huna haja ya kufikiria kununua chochote ila kama toleo hili jipya halijakufikia usiwe na wasiwasi toleo hili ndio kwanza limetoka hivi karibuni hivyo itachukua muda kidogo kufikia watu wote duniani.

Advertisement

Night Shift

Hii ni moja kati ya vilivyoongezwa kwenye toleo hili jipya la iOS 9.3 Feature hii inakusaidia kupunguza kiasi cha mwanga kwenye kioo chako kwa kufuatilia masaa pamoja na mahali ulipo. Kwa mfano kama wewe unakaribia kulala kioo cha kifaa chako cha Apple kitapunguza mwanga chenyewe Automatic ili kulinda macho yako wakati wa usiku kwani uchunguzi unasema kwamba “Kuangalia kiasi kikubwa cha mwanga angavu wa blue wakati wa jioni kunaweza kukuadhiri na kusababisha kukosa usingizi wakati wa usiku”. Hivyo kuongezeka kwa Feature hii kuatasaidia sana sio kwa ubora wa simu yako tu bali hata kiafya pia.

Health ( Afya )

Afya imekua ni sehumu kubwa ya toleo lililo pita la OS 9.. Na sasa kwenye toleo hili jipya Apple wameendela kukuletea namna rahisi ya kupata application mbalimbali kwa ajili ya afya yako ikiwa ni pamoja na namna mbalimbali zitakazo kuweza kuonyesha data mablimbali kama vile wakati unatembea, wakati unafanya mazoezi na mengine mengi data hizi zitatoka moja kwa moja katika Apple Watch.

Notes

Wote tunajua umuhimu wa application ya notes kwenye smartphone zetu kwani application hii imewezesha kupunguza matumizi ya kalamu na karatasi hasa pale unapotaka kuandika kitu ukiwa na haraka. Lakini kampuni ya Apple sasa imeleta feature mpya kwenye Application hii kwani sasa unaweza ukaweka password kwenye application hiyo ya Notes inayopatikana ndani ya simu yako.

CarPlay

Hii ni sehumu muhimu katika kila gari la kisasa duniani Feature hii inawezesha wale wenye vifaa vya magari vya apple kupata namna rahisi ya kujua sehemu kama  Gas station, Migahawa, Coffee shops na sehemu nyingine nyingi zinazo kwepo katika ramani rasmi ndani ya kifaa chako cha Apple katika gari lako. Pia sasa kwa kutumia kifaa hicho utaweza kupanga chati za muziki automatic kutokana na mapendekezo ya muziki unaopenda kusikiliza kwenye gari lako hii ikiwa ni maalumu kwa wale wenye vifaa vya apple maalumu kwaajili ya magari.

Education ( Elimu )

Apple inaweka Feature mpya ambayo itawezesha wanafunzi kushirikiana kutumia iPad, kwa mfano kama darasani kuna ipad moja tu na unataka wanafunzi watumie iPad hiyo kwa kushirikiana kila mwanafunzi anauwezo wa kuingiza password yake na kutumia iPad hiyo moja kwa kushirikiana.

  1. Kumbuka Night Shift itapatikana kwenye vifaa vya kuanzi Phone 5s na kuenelea, iPad Pro, iPad Air na kuendelea, iPad mini 2 na kuendelea, na iPod touch (6th generation).
  2. News is inapatikana U.S., UK, na Australia.
  3. Pia Toleo hili jipya pamoja na baadhi ya feature zinaweza zisipatikane kila mahali. Bonyeza hapa kuangali mahali zitakapo patikana

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use