Facebook Itasitisha Kutoa Huduma Zake kwa Watumiaji wa BlackBerry

Facebook Itasitisha Kutoa Huduma Zake kwa Watumiaji wa BlackBerry Facebook Itasitisha Kutoa Huduma Zake kwa Watumiaji wa BlackBerry

Baada ya application maarufu ya WhatsApp kusitishwa kutoa huduma zake kwa watumiaji wa BlackBerry sasa ni pigo jingine tena kwa watumiaji wa simu hizo maarufu za blackberry, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu yani 2016 Facebook imetangaza kusitisha kutoa tena huduma zake wa watumiaji wa blackberry.

Facebook ilifikia maamuzi hayo baada ya kuona kuwa blackberry ni moja kati ya OS ambazo hazitaweza tena kuwapa wateja wake mtizamo halisi unaotakiwa hii inatokana na uzamani wa OS ya Blackberry, hata hvyo mwezi November mwaka jana yani 2015 kampuni ya blackberry ilitoa smartphone yake ya kwanza inayotumia mfumo wa Android simu hiyo iliyopewa jina la BlackBerry Priv ni moja kati ya simu ya kwanza kabisa ya Android iliyotengenezwa na kampuni hiyo ya zamani ya BlackBerry.

Kwa wale watumiaji wa BlackBerry unashauriwa kutafuta simu nyingine au simu yoyote yenye uwezo wa Android au iOS kwani kwa sasa inaonekana ndipo dunia inapoelekea au kama unapenda siu za BlackBerry nunua simu mpya ya BlackBerry Priv yenye uwezo wa Android 5.0

Advertisement

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use