Sasa Unaweza kuona Idadi ya Walio Angalia Video Kwenye Instagram

Sasa Unaweza kuona Idadi ya Walio Angalia Video Kwenye Instagram Sasa Unaweza kuona Idadi ya Walio Angalia Video Kwenye Instagram

Habari njema kwa watumiaji wa Application ya Instagram, kama ulikua unajiuliza ni watu wangapi wameangalia video yako pale utakapo iweka kwenye mtandao wa Instagram ufumbuzi umepatikana. Hivi karibuni Instagram imetoa update zake mpya ambazo zitakusaidia kuona ni watu wangapi wameangalia video yako kwenye mtandao huo, kwa mojibu wa Instagram “kuona kiasi cha watu walio angalia video ni bora kuliko kuonakiasi cha walio-ipenda” alisema mmoja wa wafanyakazi katika kampuni hiyo.

Hata hivyo ukiangalia kwa upande wa watumiaje wa video kwenye Instagram ni kweli kabisa kuna watu wanaangali video lakini hawana muda wa kuipenda (kui-like) lakini unakuta ujumbe uliokusudia kuufikisha umefika kwa watazamaji wako, kwa hiyo Instagram imetoa “update” bora sana na itasaidia watumiaji wa Application hiyo kwa upande wa biashara na hata kwa wale mastaa wa hapa tanzania pamoja na waandishi wa habari.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use