Sasa Unaweza Kutuma Document Kwa Kutumia Whats App

Sasa Unaweza Kutuma Document Kwa Kutumia Whats App Sasa Unaweza Kutuma Document Kwa Kutumia Whats App

Miaka michache baada ya whatsapp kutoka mwaka 2004 na kununuliwa na kampuni ya facebook kumetokea mabadiliko mengi ya application hiyo ila sasa kuna mabadiliko mengine tena yanayo zidi kufanya whatsapp kuwa moja kati ya application za kutegemewa sana hasa hapa kwetu tanzania.

Hivi karibuni Whatsapp ilitoa toleo lake jipya ambapo sasa inakuwezesha kutuma document kwa mtu yeyote mwenye application hiyo, whatsapp imetoa toleo hilo jipya lililo pewa namba v2.12.453 kwa watumiaji wa Android na namba v2.12.4 kwa watumiaji wa iOS, hata hivyo matoleo hayo mapya kwa android na iOS yamefanya whatsapp kuongezeka vitu mbalimbali ikiwemo karibia aina mpya 100 za emojis.

Ikumbukwe pia sio watumiaji wote kwa sasa wanao-weza kupata update hiyo ila wengi wa watumiaji wa application hiyo wamesha anza kupata toleo hilo jipya na kuweza kuiona sehemu hiyo ya kutuma document, kwa sasa watumiaji waliopata toleo hilo jipya la application hiyo watakuwa na uwezo wa kutuma file za aina ya PDF tu, ila Whatsapp inategemea kuongeza aina mbalimbali za file kama DOCX na aina zinginezo kwenye siku zijazo.

Advertisement

Hata hivyo toleo hilo jipya lina onyesha kuwa sehemu hiyo ya kutuma docment itakuwa sambamba na zile sehemu zingine sita za camera na vinginevyo, ili kuona sehemu hiyo nenda kwenye application yako ya whatsapp alafu fanya kama unataka kutuma picha kisha utaona sehemu hiyo ya kutuma document ilioandikwa “Document”.

Kumbuka kwamba hauta weza kumtumia mtu document mpaka nayeye awe ame weka toleo hilo jipya la whatsapp kwenye simu yake yani Version v2.12.453 kwa watumiaji wa Android na Version v2.12.4 kwa watumiaji wa iOS.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use