Hizi Hapa Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Huawei P20

Hizi hapa ndio picha halisi za simu ya Huawei P20 inayokuja hivi karibuni
Hizi Hapa Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Huawei P20 Hizi Hapa Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Huawei P20

Hivi leo taarifa zilitoka kuhusu ujio wa simu mpya ya Huawei P20 yenye uwezo wa kamera tatu kwa nyuma, lakini kabla ya taarifa hizo hazija enea vizuri tayari tumefanikiwa kupata picha zenye muonekano wa simu hizo (ziko za aina tatu) zinazo tarajia kuzinduliwa tarehe 27 mwezi huu mwaka 2018.

Picha hizo, ambazo zimevujishwa na mvujishaji maarufu Evan Blass zinaonyesha simu hizo zikiwa na ukingo wa juu maarufu kama notch kama ilivyo simu mpya ya iPhone X.

Kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu, toleo la simu ya Huawei P20 Pro ndiyo simu inayo tarajiwa kuja na uwezo wa kamera tatu kwa nyuma. Bado mpaka sasa haijajulikana sifa zaidi za simu hizi ikiwa pamoja na uwezo wa kamera hizi. Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza yote yanayo endelea kuhusu simu hii.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use