Instagram Yaleta Sehemu ya Kutengeneza Pesa Kupitia IGTV

Hatimae jiandae kuanza kutengeneza pesa kupitia mtandao wa Instagram
Instagram Yaleta Sehemu ya Kutengeneza Pesa Kupitia IGTV Instagram Yaleta Sehemu ya Kutengeneza Pesa Kupitia IGTV

Baada ya tetesi za mtandao wa Instagram hivi karibuni kuleta njia mpya ya kutengeneza pesa kwa wabunifu wake kupitia sehemu ya IGTV, hatimaye sehemu hiyo yatangazwa rasmi. IGTV ni sehemu ya mtandao wa Instagram ambayo inaruhusu watumiaji kuweka video ndefu zenye zaidi ya dakika moja tofauti na video za kawaida ambazo huwa zimezoleka kuwa na secunde 60 au dakika moja.

Tangu sehemu hiyo ya IGTV ilipoanzishwa mwaka 2018 kulikuwa hakuna njia yoyote ambayo wabunifu wanaweza kufaidika na video ndefu wanazo pakia kupitia sehemu ya IGTV.

Lakini hivi karibuni wabunifu wote duniani wanaweza kuanza kufaidika na video zao kupitia matangazo yatakayo anza kupita kwenye video zao za IGTV.

Advertisement

Matangazo hayo yatakuwa yanafanya kazi kama matangazo ya YouTube na mtazamaji ataweza kuona tangazo pale atakapo bofya kitufe cha kuangalia video nzima baada ya kuangalia preview kwenye uwanja wa post za kawaida.

Kama ilivyo kwenye mtandao wa YouTube, pia utaweza kurusha tangazo au Skip Ad na kuangalia video husika moja kwa moja. Hata hivyo kwa mujibu wa Instagram, video hizo ambazo zitakuwa zikipita kama matangazo zitakuwa na urefu wa hadi sekunde 15.

Kama ilivyo kwenye mitandao mingine, mbunifu ataweza kulipwa kutokana na watu walio tazama matangazo na pia kwa idadi ya watu walio bofya matangazo yanayopita kwenye video husika. Hata hivyo kwa mujibu wa CNBC, Instagram itagawana mapato na wabunifu wote watachukua takribani asilimia 55 ya mapato.

Kuhusu upatikanaji wa sehemu hiyo, Instagram imetangaza kuwa kwa sasa sehemu hiyo inategemea kuanza kufanya kazi kwa wabunifu wa nchini marekani na baadae kuanza kusambaa kwa wabunifu kwenye nchi mbalimbali duniani kote.

Mbali na matangazo ya IGTV, pia instagram imetangaza kuja na njia nyingine ya wabunifu kupata pesa ambayo itasaidia zaidi wabunifu kutoka nchi za ugaibuni. Sehemu hiyo mpya itakuwa inawapa furasa watumiaji kuchangia kiasi cha pesa kupitia stika maalum ambazo mtazamaji anaweza kununua wakati mbunifu huyo yupo Instagram Live.

Instagram Yaleta Sehemu ya Kutengeneza Pesa Kupitia IGTV

Kama unavyoweza kuona, mwisho kabisa wa uwanja wa Instagram Live utaweza kuona sehemu iliyoandikwa “Buy a badge to support”. Sehemu hiyo itakuwa inaonekana wakati wote mbunifu atakapo kuwa akionyesha video yake ya Live kupitia Insta Live.

Kwa mujibu wa Instagram sehemu hii ita anza kufanyiwa majaribio na kwa watu wachache na baadae kuanza kufanya kazi mwezi ujao kwa watumiaji wa nchi za Amerika, Brazil, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Uturuki, Hispania, na Mexico. Kwa sasa bado hatuna uhakika kama sehemu hii itakuja kwenye nchi za Afrika hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use