Sehemu Mbili Mpya Kwenye Instagram Ambazo Ulikuwa Huzijui

Sehemu hizi zitafanya akaunti yako kuwa ya kipekee kabisa
Sehemu Mbili Mpya Kwenye Instagram Ambazo Ulikuwa Huzijui Sehemu Mbili Mpya Kwenye Instagram Ambazo Ulikuwa Huzijui

Mtandao wa Instagram umekuwa ukiongezewa sehemu mpya kila siku, sehemu nyingi zimekuwa zikigundulika kabla ya kufikia kwenye app hiyo na nyingine huwa zinaongezwa bila mtu yoyote kujua au bila taarifa ujulikana kwa watu wengi.

Kuliona hili leo nimekuletea sehemu mbili mpya kwenye mtandao wa instagram, ambazo huwenda ulikuwa huzijui hadi leo. Kumbuka sehemu hizi tayari zipo kwenye mtandao huo hivyo unaweza kufuta hatua hizi kuweza kujua jinsi ya kuwasha sehemu hizo. Basi bila kupoteza muda twende tukaangalie sehemu hizi.

Tangeneza Password Moja ya Akaunti Zako Zote

Hivi karibuni instagram imeleta sehemu mpya ambayo itakusaidia kutengeneza password moja ambayo itakusaidia kuingia kwenye akaunti zako zote. Sasa kama wewe ni mtu mwenye akaunti zaidi ya moja basi sehemu hii itakusaidia sana. Ili kuwasha sehemu hii ingia kwenye Settings kisha mwisho kabisa wa ukurasa huo chagua sehemu iliyoandikwa Set up Multi-Account Login.

Advertisement

Sehemu Mbili Mpya Kwenye Instagram Ambazo Ulikuwa Huzijui

Baada ya hapo bofya Continue, kisha utaplekwa kwenye ukurasa unao kuitaji kuchagua akaunti ambayo ndio itakuwa imeshikilia akaunti zako zote. Baada ya hapo bofya Next na kisha utafunguka ukurasa juu yake bofya OK, Baada ya hapo utaletewa ukurasa ambao unatakiwa kuchagua akaunti unazotaka ziwe zinafunguliwa na akaunti hiyo, weka vidoti vya tiki kwenye kila akaunti kisha malizia kwa kubofya Next alafu bofya Done.

Kuanzia hapo kila utakapokua unaingia kwenye akaunti yako moja basi akaunti zingine zote zitajiweka moja kwa moja. Hii ni nzuri kwa wale watu wenye akaunti nyingi na inasaidia sana kama utakuwa unasahau password mara kwa mara.

Akaunti Mpya za Watu Maalum

Kwenye mkutano wa F8, Facebook ilitangaza kuleta akaunti za watu maalum kwa watumiaji wote wa mtandao wa Instagram. Awali akaunti hizi zilikuwa ni maalum kwa watu walio chaguliwa na instagram lakini sasa akaunti hizo zinapatikana kwa watumiaji wote.

Kama wewe ni mtu maalum au unafanya kazi maalum basi unaweza kubadilisha akaunti yako ya Instagram kuwa ya mtu maalum. Unaweza kufanya hivyo kwa kubofya sehemu ya Settings kisha bofya sehemu ya Account kisha bofya Switch to Creator Account, baada ya hapo utaletewa ukurasa wenye kutaja faida za ukurasa wa mtu maalum kisha bofya Next.

Sehemu Mbili Mpya Kwenye Instagram Ambazo Ulikuwa Huzijui

Baada ya hapo kama wewe ni mwanasheria andika Lawyer kwenye sehemu ya kutafuta, kisha chagua Lawyer. Kama wewe ni blogger kama mimi basi andika blogger kwenye sehemu ya kutafuta, vilevile fanya hivyo kulingana na aina ya kazi unayofanya. Baada ya hapo kama bado huna akaunti ya Facebook, kupitia ukurasa huo utaweza kutengeneza ukurasa mpya kwaajili ya akaunti yako hiyo.

Na hizo ndio sehemu mbili ambazo naamini ulikuwa huzijui kwenye akaunti yako ya Instagram, kama makala hii imekusaidia unaweza kutuambia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa habari zaidi na maujanja mbalimbali hakikisha unaendelea kutembekea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use