Huawei Kuja na Simu Mpya Yenye 5G Mwaka Ujao 2019

Simu yenyewe inasemekana itakuwa ni Huawei Mate 30
Huawei 5G Huawei 5G

Wakati hapa Tanzania kampuni nyingi za simu zikiwa bado hazina mtandao bora wa 4G, nchi nyingine wameanza mkakati wa kuanza kutumia mtandao wa 5G ambao unasemekana kuwa na kasi zaidi.

Kuliona hilo kampuni ya Huawei imetangaza rasmi kuwa itakuwa tayari kutoa simu yake ya kwanza inayo tumia mtandao wa 5G mara ifikapo nusu ya pili ya mwaka 2019, hata hivyo Huawei imesema pia inategemea router ya kwanza ya Huawei yenye uwezo wa 5G kutoka kwenye robo ya kwanza ya mwaka 2019.

Huawei imekuwa ni moja kati ya kampuni zinazo shindana sana kiteknolojia kwani mwaka huu Huawei ilizindua simu za Huawei P20 na P20 Pro simu zinazo tabiriwa kufanya vizuri sana kwa mwaka huu kwa sababu ya mfumo wake wa kamera unao tumia AI au Artificial intelligence.

Advertisement

Kwa sasa ripoti kuhusu ujio wa vifaa hivyo vyenye 5G kutoka Huawei zinasema kuwa, simu hiyo ya kwanza itakayokuja na uwezo wa 5G itakuwa ni simu ya Huawei Mate 30 ambayo ndio imekuwa na utaratibu wa kuzinduliwa na Huawei kwenye kila nusu ya pili ya kila mwaka. Hata hivyo kwa sasa bado tunasubiri Huawei Mate 20 ambayo nayo inatazamiwa kutoka kwenye nusu ya pili ya mwaka huu 2018 ambayo inaanza mwezi July, 2018.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use