Galaxy S7, A3, A5 na A7 Kupata Toleo la Android 8 Mwezi May

Kama unatumia simu hizo tegemea toleo la Android Oreo Kuanzia mwezi May
Samsung-Galaxy-S7-Edge Samsung-Galaxy-S7-Edge

Hivi karibuni watumiaji wengi sana wanaotumia simu za Android wamekuwa wakitamani kupata toleo jipya la Android 8 au Android Oreo kwenye simu zao za Android. Lakini kwa watumiaji wa simu za Samsung ni wazi kuwa kampuni ya Samsung imekuwa taratibu sana kutoa matoleo mapya ya Android kwenye simu mbalimbali za Android na kufanya watumiaji kusubiri kwa muda mrefu sana.

Japokuwa hivi karibuni tulipata list ya simu za Samsung ambazo zinaweza kupata kupata toleo la Android Oreo, lakini vilevile kwenye list hiyo ni baadhi ya simu tu ambazo tayari zimepata toleo hilo la Android Oreo. Lakini sasa kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, kama wewe ni mmiliki wa simu za Samsung Galaxy S7, Galaxy A3 (2017), Galaxy A5 (2017), pamoja na Galaxy A7 (2017) basi tegemea kupata toleo jipya la Android Oreo au Android 8.0 siku za karibuni.

Ripoti hizo pia zinabainisha tarehe halisi ya kutoka kwa toleo hilo ni kuanza tarehe 18 May na simu za Galaxy S7 na S7 Edge ndizo zitakuwa za kwanza kupata toleo hilo ikifuatiwa na Simu nyingine kwenye list hii za A3, A5, alafu A7 zote zikiwa ni simu za mwaka 2017.

Advertisement

Hata hivyo inawezekana kuwa toleo hilo likachelewa kidogo kwa Tanzania, hivyo kama wewe ni mtumiaji wa simu hizo na upo Tanzania au Afrika mashariki kwa ujumla tegemea toleo hilo ndani ya mwezi wa tano mwaka huu 2018 au mwanzoni mwa mwezi wa sita mwaka huu 2018.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use