Movie za Teknolojia za Kuangalia Kipindi Hichi cha Sikukuu

Movie nzuri ambazo unaweza kuangalia kipindi hichi cha sikukuu
Movie za Teknolojia za Kuangalia Kipindi Hichi cha Sikukuu Movie za Teknolojia za Kuangalia Kipindi Hichi cha Sikukuu

Kama wewe ni kama mimi najua najua unapenda kuangalia movie sana, lakini kama hii ni mara yako ya kwanza basi ningependa ujaribu kuangalia angalau Movie moja kwenye list hii kisha ukimaliza uje uniambie umeonaje movie kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Kutokana na kuwa Tanzania Tech ni tovuti ya teknolojia, nitajitahidi kuwa ndani ya mada na kutaja filamu au movie nyingi ambazo zinahusu teknolojia, kumbuka unaweza ukakuta movie mbili, tatu ambazo azihusu teknolojia kutokana na kuwa aiseeee… ni movie nzuri na imeshindikana kuandika makala hii bila kuzitaja movie hizo, basi bila kupoteza muda zaidi twende tukangalie Movie hizi.

Alita

Advertisement

Alita ni Movie inayohusu maisha ya daktari au mtaalamu wa teknolojia ambaye alikuwa na uwezo wa kutengeneza au kuunda roboti mbalimbali. Mtaalamu huyo alifanikiwa kuokota sehemu ya kichwa cha roboti ambaye anajulikana kwa jina Alita, daktari huyo anatengeneza roboti hiyo na kuipa mwili bila kujua kuwa roboti hiyo inauwezo mkubwa kuliko alivyodhani.

Download Hapa

Escape Room

Escape Room ni movie inayohusu maisha ya watu watano ambao maisha yao yalikubwa na mikosi kwa kipindi cha nyuma, watu hao wanaonekana kuendelea na maisha yao hata baada ya mikosi hiyo lakini baadae wanapewa mialiko ya kujumika kwenye mchezo ambao ukishinda unapewa dollar za marekani milioni 1, bila kujua kuwa mchezo huo ni mchezo wa kifo.

Download Hapa

Gemini Man

Gemin Man ni movie inayohusu mdunguaji (Sniper) mwenye uwezo mkubwa wa kudungua hata mahali pasipo wezekana kikawaida, mdunguaji huyo baadae anakuja kugundua kuwa kazi alizokuwa anapewa na wajiri wake sio kuuwa majangili bali ni kuuwa watu wasiokuwa na hatia. Wajiri wake wana amua kumuua yeye na timu yake baada ya kuona amengundua hilo.

Download Hapa

Line of Duty (2019)

https://youtu.be/OiKzf4EF7xk

Line of Duty ni movie inayohusu polisi na mwandishi wa habari ambao wanajikuta wakiangaika kwa pamoja kumtafuta mtoto wa inspecta wa polisi ambaye alikuwa akishiliwa na majangili. Mwandishi wa habari huyo alikuwa akiangaika kutafuta habari bila kujua anajingiza kwenye upepelezi uliokuwa unafanywa na polisi.

Download Hapa

Captain Marvel

Kama hadi sasa bado hujaangalia movie hii basi nadhani nachoweza kukuliza ni kuwa UNASUBIRI NINI..? sina haja ya kukwambia movie hii inahusu nini bali nadhani itabidi utafute movie hii mwenyewe na ungalie maana ukweli umeniudhi kwa sababu kwanini hujangalia movie hii hadi sasa..? ahh. Anyway Movie hii ni nzuri sana guys na ni nyepesi kuelewa hasa kama umeangalia The Avengers.

Download Hapa

Code 8

Code 8 ni Movie inayo muhusu kijana mmoja mwenye nguvu za ajabu ambaye anapambana na sheria baada ya kufanya uhalifu kutokana na kukosa kazi kwa muda mrefu. Kijana huyo najikuta kwenye utata mkubwa kati ya polisi na watu wengine wenye nguvu za ajabu.

Download Hapa

List inaendelea…

Kama umependa awamu hii ya kwanza ya basi hakikisha una toa maoni yako hapo chini ili kusudi tuendelee na awamu ya pili ambapo tutaongeza list hii ya movie nzuri ambazo unaweza kuangalia kipindi hichi cha sikukuu. Hakikisha unatoa maoni hapo chini kama unataka tuongeze list hii au kama wewe ni mpenzi wa filamu unaweza kusoma list ya mwaka 2018 hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use