Kama wewe ni mpenzi wa mchezo wa mpira wa miguu basi najua lazima unajua kuwa michuano ya La Liga imesha anza rasmi. Kwa upande wetu hapa Tanzania Tech ni wakati mwingine ambao tunaenda kuangalia apps nzuri ambazo zinaweza kukusaidia kufuatilia michuano ya La Liga.
Basi bila kupoteza muda twende tukaangalie App hizi nzuri ambazo na uhakika kabisa lazima zitakusaidia kupata matokeo na habari zote muhimu kuhusu michuano hiyo ya La Liga.
1. La Liga – Spanish Soccer League Official
- Android
- iOS
Kama wewe ni mpenzi wa ligi hii basi ni muhimu kuhakikisha kuwa unayo app ya La Liga kwenye simu yako. App hii itakupa uwezo wa kupata habari mbalimbali pamoja na matokeo ikiwa na ratiba za michezo mbalimbali moja kwa moja kwenye simu yako ya Android na iOS.
2. Onefootball – Soccer Scores
- Android
- iOS
Mbali ya kuwa na uwezo wa kukupa habari za michuano ya La Liga App hii itakupa uwezo wa kukupa habari mbalimbali kuhusu mpira wa miguu. App hii ni nzuri sana na ukweli ni kuwa unaweza kuendelea kutumia app hii kwa muda mrefu hata baada ya kuisha kwa michuano ya La Liga.
3. All Football – Latest News & Videos
- Android
- iOS
App nyingine bora ambayo itakupa habari mbalimbali za michuano ya La Liga ni App hii ya All Football. Najua kama wewe ni mpenzi wa michezo ya mpira wa miguu lazima utakuwa unaijua app hii, basi sidhani kama ninahaja ya kusema zaidi kuhusu app hii.
4. La Liga TV – Official soccer channel in HD
- Android
- iOS
App nyingine nzuri ambayo unaweza kutumia kipindi hiki cha michuano ya La Liga ni App ya La Liga TV. App hii ni nzuri sana na itakusaidia kuweza kuangalia michuano hiyo Live pamoja na kupata habari mbalimbali za timu unayoipenda.
5. La Liga – 90min Edition
- Android
- iOS
App nyingine nzuri ya kufuatili kombe ya La Liga ni App ya La Liga 90min, app hii ni nzuri sana na itakupa habari zote ambazo zinahusu timu unayoipenda pamoja na habari za michuano hiyo kwa ujumla. App hii kama zilivyo nyingine kwenye list hii inapatikana kwenye mifumo yote ya Android na iOS.
Na hizo ndio app nilizo kuandalia kwa siku ya leo, kama unataka kujua app nyingine nzuri unaweza kusoma makala yetu iliyopita ya App nzuri. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.