in

Apps# 20 App Nzuri za Kujaribu Kwenye Simu ya Android

Usihahau kuangalia app ya mwisho kabisa kwenye list hii

App nzuri za Android Kujaribu

Kama wewe ni msomaji wa mara kwa mara wa tovuti ya Tanzania Tech, lazima utakuwa unajua kuhusu apps mbalimbali tunazo ziangalia hapa kwenye makala za Apps nzuri, kama unavyoweza kuona kichwa cha habari hapo juu hii ni sehemu ya 20 au makala ya 20 ya app nzuri hivyo unaweza kusoma makala zilizopita na kujua app nyingine nzuri kwaajili ya simu yako.

Wiki hii pia nimekuandalia app nyingine nzuri ambazo najua kwa namna moja ama nyingine zinaweza kurahisisha matumizi yako ya simu yako ya Android au kufanya ufurahie zaidi simu yako, basi bila kupoteza muda twende tukangalie app hizi nzuri.

1. Hide – Blue Ticks or Last Seen, Photos and Videos

Kwa kuanza tuanze na app ya Hide, App hii ni nzuri sana kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp kwa simu za Android, app hii itakupa uwezo wa kusoma meseji ulizo tumiwa bila kuonyesha kama umesoma meseji hizo pia bila kuweka tiki za blue. Vilevile unaweza kutumia app hii kuangalia video ulizotumiwa bila aliye kutumia kuweza kuona app hii ni nzuri sana hivyo nakushauri ujaribu sasa.

2. Social toolbox – ? for Instagram

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda akaunti za instagram kuonekana vizuri basi utaipenda app hii ya Social toolbox, app hii inakupa effect au vikorombwezo mbalimbali vya picha kwaajili ya picha zako za instagram na kufanya picha zako kushangaza watu wengi. App hii ni nzuri sana kwa watu wenye akaunti za instagram wanapenda akaunti zao zionekane kisasa zaidi.

Apps (7) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2022)

3. Navigation Gestures – Swipe Gesture Controls!

Navigation Gestures ni app nyingine nzuri kwaajili ya kurahisha matumizi ya simu yako ya Android. App hii inakupa uwezo wa kubadilisha vitufe vya kurudi nyuma na kitufe cha katikati kuwa kama ilivyokuwa kwenye mfumo wa simu nyingi za sasa za android pamoja na iOS. Kupitia app hii utaweza kuweka sehemu ya mstari chini ya kioo chako na utaweza kutumia mastari huo kwenda mbele na kurudi nyuma kwenye simu yako.

4. Hi Translate – Whatsapp translate, Chat Translator

Hi Translate ni app nzuri sana kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp, app hii inakupa uwezo wa kutafsiri maneno unayotumiwa wakati unachati na mtu kwa kutumia programu ya WhatsApp, app hii pia inaweza kukusaidia kutafsiri maneno kwa haraka zaidi kwenye simu yako kwa kushikilia neno unapotaka kutafsiri.

5. World Around Me

World Around Me
Price: Free

World Around Me ni app nyingine nzuri ya Android ambayo inaweza kukusaidia sana kupata sehemu mpya za kutembelea kwa haraka zaidi. Kama wewe ni mpenzi wa kutembelea sehemu mpya iwe hotel, migahawa na hata sehemu nyingine za muhimu app hii ni nzuri sana kwako, App hii inatumia kamera ya simu yako kuweza kuonyesha mahali au sehemu ambapo zinapatikana sehemu mpya kwenye eneo ulilopo, unachotakiwa kufanya ni kuwasha app hii kisha washa GPS kisha chagua mahali iwe ATM, au Hotel app hii itaweza kuonyesha upande sehemu hizo zilipo pamoja na kukupa maelezo ya muhimu kuhusu sehemu hizo.

Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted

6. Tanzania Tech Forums (Beta)

Kama unavyoweza kuona Jina hapo juu hii ni app mpya kabisa kwaajii ya wasomaji wa Tanzania Tech, App hii itakupa uwezo wa kuuliza maswali na kupata majibu moja kwa moja kwa kutumia simu yako ya Android. App hii bado iko kwenye hatu za majaribio hivyo ni matumaini yetu tutaendelea kuleta sehemu mpya kwenye app hii pamoja na kuiboresha zaidi.

Na hizo ndio app tulizo kuandali kwa siku ya leo, unaweza kusoma hapa app nyingine nzuri kupitia makala yetu iliyopita na uhakika utapata app nyingine nzuri kwaajili ya kurahisha matumizi yako ya kila siku ya simu yako ya Android.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment