Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Menu za Siri Kwenye Simu Yako ya Android

Utaweza kujua menu ambazo hazikuwa zinaonekana wazi kwenye simu yako
Zifahamu Menu za Siri Kwenye Simu Yako ya Android Zifahamu Menu za Siri Kwenye Simu Yako ya Android

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android ni wazi hadi sasa unahisi unaijua simu yako. Lakini naomba nikwambie ukweli kuwa “teknolojia haina mjuzi asilimia 100″ kwani ni wazi kuwa hata wewe uwe mtaalamu kiasi gani ni lazima kuna kitu utakuwa haufahamu ambacho mtu mwingine anakijua.

Sasa kuliona hilo leo nataka niongeze list ya vitu ambavyo unavijua vinavyo husiana na teknolojia ikiwa pamoja na simu yako kwa ujumla. Kupitia makala hii nitaenda kushare na wewe njia rahisi sana ambayo unaweza kujua Menu za siri zilizopo kwenye simu yako ya Android.

Advertisement

Menu hizo nyingi zipo kwa siri kwenye simu yako kwa sababu sio mara zote umekuwa ukizihitaji hasa kama wewe ni mtumiaji wa simu wa kawaida. Lakini kama wewe ni kama mimi na unapenda kujifanya unajua kila kitu ni wazi kuwa huwenda menu hizi za kawaida zisiwe zinatosha kwako.

Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye hatua hizo. Kitu cha kwanza ambacho ni muhimu hakikisha unapakua app hapo chini.

Download Hapa

Baada ya kupakua app hiyo moja kwa moja fungua app hiyo, na mara baada ya kufungua kisha subiria kwa sekunde chache app hiyo itafute menu za siri kwenye simu yako, baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuziona kwenye kioo cha simu yako.

Zifahamu Menu za Siri Kwenye Simu Yako ya Android

Kulingana na simu yako, unaweza kukutana na mamia ya menu za siri ambazo unaweza kubofya moja baada ya nyingine kujua menu hiyo inafanya nini. Kuna menu nyingine ni maalum kwa ajili ya sehemu zilizo fichwa kabisa ndani ya simu yako na hivyo zinaweza zisifunguke mpaka simu yako iwe rooted.

Zifahamu Menu za Siri Kwenye Simu Yako ya Android

Lakini pia unaweza kukutana na menu za kawaida zilizoko ndani ya simu yako kwani app hii ukusanya menu zote za siri na zile ambazo sio za siri kwenye sehemu moja.

Zifahamu Menu za Siri Kwenye Simu Yako ya Android

Pia kama wewe unajua kitu chochote ambacho unataka kujua kama kipo kwenye simu yako basi unaweza kutumia sehemu ya kutafuta kuweza kutafuta menu yake hata kama imefichwa. Kwa mfano unaweza kutafuta “dark mode”, au “screen mode” au chochote kile.

Zifahamu Menu za Siri Kwenye Simu Yako ya Android

Mbali na hayo, pia unaweza kutumia app hii kama mbadala wa settings kwenye simu yako kwani inakurahishia kufungua settings fulani kwa haraka zaidi, fikiri app hii kama “command prompt” kwenye kompyuta yako.

Basi kwa kufuata hatau zote hapo juu natumaini utakuwa umeweza kujua baadhi ya menu za siri ambazo huwenda ulikuwa huzijui kabla. Kama kuna mahali utakuwa umekwama basi unaweza kuwasiliana nasi kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tuna ahidi kukusaidia.

Kama unataka kujua maujanja zaidi unaweza kusoma hapa makala yetu iliyopita ambayo tumeonyesha jinsi ya kupata code za siri zenye uwezo kwa kufanya mambo mbalimbali kwenye simu yako ya Android.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use