Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

HyperDrive Kifaa cha Kuongeza Port Kwenye MacBook Pro

Kifaa hichi kinauwezo wa kukusaidia uweze kutumia port za kawaida kwenye MacBook Pro ya mwaka 2016
HyperDrive HyperDrive

Kama tunavyojua MacBook Pro ya mwaka 2016 inakuja na aina mpya ya port ambazo hizi zinatofautiana sana na zile port za kawaida za USB ambazo tunazitumia kila siku. Kukosekana kwa port hizi kumefanya watumiaji wengi sana kuwa na vifaa vya kuunganisha (dongle) ili kutumia port hizo zilizo zoeleka.

Kutokana na ukosefu wa port hizo, matumizi ya vifaa hivyo yamekuwa makubwa sana ukizingatia MacBook hiyo ya mwaka 2016 haitumii kabisa port za kawaida au zilizo zoeleka. Ili kupunguza matumizi hayo ya vifaa vingi kampuni ya HYPER yenye makao makuu huko San Francisco, CA imegundua kifaa kipya kitanachoitwa HyperDrive.

Advertisement

Kifaa hichi cha HyperDrive kina uwezo wa kufanya kompyuta yako ya MacBook Pro ya Mwaka 2016 kutumia port za kawaida za USB, HDMI na nyingine nyingi. Kwa sasa kifaa hichi kipo kwenye hatua za ambapo watengenezaji wake wanaomba msaada ili kumalizia kifaa hicho, kama unataka kutoa msaada unaweza kutembelea tovuti ya Kickstarter.com.

Kifaa hicho kwa sasa kinauzwa kwa dollar za marekani $49 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 110,000 lakini bei hiyo ni kupitia page yao iliyoko kwenye tovuti ya Kickstarter.com ambayo husaidia wajaria mali kupata msaada kutoka kwa watu mbalimbali ili kufanikisha kuingiza bidhaa zao sokoni.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania tech au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use