Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tumia Internet ya Simu Moja Kwenda Nyingine Kupitia Link

Sasa acha kutumia watu password za Hotspot kwani unaweza kutumia link
Tumia Internet ya Simu Moja Kwenda Nyingine Kupitia Link Tumia Internet ya Simu Moja Kwenda Nyingine Kupitia Link

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapendelea kutumia internet ya simu yako na ndugu jamaa au marafiki basi pengine njia hii inaweza kuwa bora zaidi kwako. Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ya kushare internet kwa kutumia link maalum na sio password kama ilivyo zoeleka na watu wengi.

Najua hata wewe umesha zoea kuwa unapo washa Hotspot nilazima mtumiaji anaetaka kujiunga na internet hiyo awe na password. Lakini naweza kukwambia kuwa sio lazima kutumia password kwani unaweza kushare internet na marafiki zako kwa kutumia link maalum na sio password.

Advertisement

Kupitia njia hii utaweza kushare internet yako kwa urahisi kwa kushare tu link na moja kwa moja mtu wa pili ataweza kutumia internet yako bila yeye kuingiza password ya aina yoyote. Basi bila kupoteza muda twende kwenye makala hii..

Hatua ya Kwanza – Download App kupitia link hapo chini, kama link hiyo haifanyi kazi kwenye simu yako basi unaweza kutumia link hapo chini.

WifiLink: Share WiFi
Price: Free

Download App Hapa (Android)

Download App Hapa (iOS)

Hatua ya Pili – Baada ya kumaliza kuinstall app hii vizuri kwenye simu yako sasa fungua app hii kisha fuata maelezo na baada ya hapo bofya sehemu ya hotspot iliyopo chini.

Tumia Internet ya Simu Moja Kwenda Nyingine Kupitia Link

Hatua ya Tatu – Andika jina kwenye sehemu ya Network Name, kisha kwenye sehemu ya password andika password yako na kisha bofya Share Link.

Tumia Internet ya Simu Moja Kwenda Nyingine Kupitia Link

Tuma link kwa ambaye unataka kushare nae Internet yako kisha atakapo pata link hiyo moja kwa moja ataweza kujiunga na Internet yako bila ya kuwa na password. Kumbuka, anae pokea link hiyo naye anatakiwa kuwa na app hiyo kwenye simu yake hivyo hakikisha na yeye anapakua app hiyo kwanza.

Kwa kufuata hatua hizi chache bila shaka utaweza kushare internet yako kwa urahisi na haraka kwa kutumia link. Kumbuka njia hii ni nzuri na unaweza kushare internet yako kwa haraka kuliko kushare password zako kila mara.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa YouTube hapa. Kama unataka kujifuza zaidi unaweza kusoma hapa kujua mtu ambaye anachati sana na mtu wako wa karibu bila wewe kujua.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use