Jinsi ya Kutengeneza Beat Kupitia Simu ya Android

Jifunze jinsi ya kutengeneza beat kwa kutumia apps hizi nzuri
Jinsi ya Kutengeneza Beat Kupitia Simu ya Android Jinsi ya Kutengeneza Beat Kupitia Simu ya Android

Wote tunapenda muziki lakini wapo wale wanaopenda zaidi kutengeneza muziki kiasi kwamba wanapenda hadi kutengeneza muziki au beat kupitia simu zao za mkononi. Well.. kama wewe ni mmoja wa watu hao basi makala hii ni kwa ajili yako.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia Apps nzuri za kusaidia kutengeneza beat moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi, kwa kuanza siku ya leo tutaangalia Apps za Android na makala nyingine itakayokuja itakuwa kwa ajili ya watumiaji wa simu za mfumo wa iOS.

Basi bila kupoteza muda let’s get to it.

Advertisement

FL STUDIO MOBILE
Price: $14.99

Kama kwa namna yoyote umeshawahi kujaribu kutengeneza muziki au beat basi lazima unajua kuhusu Fruit Loop Studio, programu hii ni maarufu sana na imekuwa ikitumiwa na watayarishaji wengi sana kutayarisha muziki bora ambao kila siku unasikiliza kupitia radio au tv yako. Sasa programu hii inakuja na programu ya Android ambayo kwa bahati mbaya inapatikana kwa kulipia kwenye soko la Play Store. Lakini unaweza kutembelea tovuti hapa kujua jinsi ya kupata programu hiyo bila kulipia.

Download App Hapa

Hip Hop Pads
Price: Free

Kama wewe ni mpenzi wa kutengeneza muziki hasa wa hip hop basi App hii ni nzuri kwako. App hii inakuruhusu kutengeneza beat moja kwa moja kwenye simu yako kwa kugusa vitufe mbalimbali vilivyopo kwenye app hiyo, kama unataka kuwa maatalam wa kutengeneza beat kupitia njia rahisi basi nakushauri kuanza na app hii kwani ni rahisi kutumia na inakupa uwezo wa kutengeneza beat hasa za hip hop kwa urahisi na haraka.

Download App Hapa

Drum Pads 24 ni app nyingine nzuri kwa wapenzi wa kutengeneza beats, App hii ina fanana na app iliyopita ila hii inautofauti kidogo, app hii imechanganya na kick pamoja na drums hivyo kama unataka kutengeneza muziki wenye ngoma ndani yake basi app hii ni nzuri sana kwako.

Download App Hapa

Kama umefanikiwa kudownload na kujaribu app hiyo hapo juu basi lazima ujaribu na app hii ya Hip Hop Drum Pads 24, app hii ni kama iliyopita lakini hii ni bora zaidi pale inapokuja kwenye swala zima la kuchanganya beat ili kupata muziki bora.

Download App Hapa

Kama wewe ni mpenzi wa kutengeneza beat au muziki kupitia simu ya Android basi nadhani ni lazima kujaribu app hii ya Music Maker Jam. App hii ni bora sana kwa sababu inakuja na njia nyingi za kutengeneza muziki wa aina mbalimbali kama vile Rock, Hiphop, R&B, Techno na muziki wa aina nyingine nyingi, kitu kizuri ni kuwa app hii ni rahisi sana kutumia na inakuja na sehemu nyingine nyingi za kusaidia kuedit muziki kwa haraka.

Download App Hapa

Kwa sababu najua wewe ni mpenzi wa muziki basi app hii sio kwa ajili ya kutengeneza muziki bali itakusaidia sana kuweza kupata beats za kufanyia mazoezi kwa urahisi kabisa. App hii inakuja na beats mbalimbali ambazo unaweza kuzutumia kufanya mazoezi ili kuweza kujua ni aina gani ya muziki uweze kutengeneza, hii ni app nzuri sana na japo kuwa mimi sio mpenzi wa kutengeneza muziki lakini ninayo app hii kwenye simu yangu.

Download App Hapa

Kwa mapendekezo yangu hizi ndio apps nzuri za kutengeneza beats au muziki kupitia simu ya Android. Kumbuka zipo apps nyingi sana za kutengeneza beats kupitia soko la Play Store hivyo unaweza kuwa unajua apps nyingine ambazo ni bora zaidi ya hizi hivyo unaweza kutujuza kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tutaongeza app hiyo kwenye list hii moja kwa moja.

Kama unataka kujua apps nyingine nzuri za kusaidia kubadilisha sura ya kwenye picha zako kuwa kama ya mzee kama inavyofanya kazi app ya FaceApp basi unaweza kusoma hapa. Kwa habari zaidi kuhusu teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Pia hakikisha una subscribe kwenye channel yetu kupitia YouTube kwani kuna kitu kikubwa kinakuja hivi karibuni.

3 comments
  1. Ok nimeipenda sana app hii na pia nina penda kazi hi ya mziki .nakilichokuwa kinanisumbua kupata angalau beat ya kujifunzia .naiman sasa nitaweza nataman kufika mbali bip up sana endeleeni kutujuza

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use