Tumia (AI) Artificial Intelligence Kupata Likes Nyingi Instagram

Njia rahisi ya kupata likes kwa kutumia mfumo wa (AI) Artificial Intelligence
Tumia (AI) Artificial Intelligence Kupata Likes Nyingi Instagram Tumia (AI) Artificial Intelligence Kupata Likes Nyingi Instagram

Kama wewe ni msomaji wa Tanzania tech ni wazi kuwa umesha jifunza mambo mengi kuhusu AI au Artificial intelligence. Kupitia makala hii tutaenda kuangalia zaidi njia za kutumia AI kupata likes nyingine kwenye akaunti yako ya Instagram.

Kumbuka njia hii inafanya kazi zaidi kama unataka likes na sio followers, kama unataka followers basi unaweza kusubiri makala yetu nyingine.

Kwa kuanza moja kwa moja hakikisha unafuata amaelezo kwenye video hapo chini mwanzo hadi mwisho na utaweza kupata likes nyingi kwenye akaunti yako kwa kutumia mfumo wa AI.

Advertisement

Unacho takiwa kufanya ni kupakua app hapo chini, app hii ni tofauti kabisa na app nyingine ambazo umewahi kusikia.

App hii inatumia mfumo maalum wa AI kuweza kujua ni aina gani ya hashtag ambazo unatakiwa kutumia kwenye picha au video ili kufikia watu wengi zaidi. Unaweza kupata app hiyo hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kupakua app hii sasa endelea kwa kufungua app hiyo kisha endelea kwa kuchagua maneno, au picha au link ya post ili kupata hashtag.

Sehemu bora ni sehemu ya katika ambayo ni Photo, bofya hapa na kisha bofya “New Photo” alafu chagua picha ambayo unataka kupost kwenye akaunti yako ya Instagram alafu subiri baada ya muda app hiyo itakwambia ni hashtag gani ambazo ni bora kwako kutumia kwenye picha hiyo.

Kwa maelezo rahisi zaidi na bora angalia video hapo juu.

Tumia (AI) Artificial Intelligence Kupata Likes Nyingi Instagram

Baada ya hapo kupata matokeo mazuri, copy hashtag ambazo zinatokea kwenye sehemu ya medium na sehemu ya Easy na kwenye sehemu ya hard copy hashtag moja tu.

Hii ni kwa sababu hashtag za hard ni ngumu kufikia watu wengi kutokana na kutumiwa na watu wengi sana na hashtag nyingine ni rahisi kwani hazitumiwi na watumiaji wengi.

Kama unataka kucopy hashtag, bofya hashtag unazo zitaka kisha moja kwa moja bofya kutufe cha copy kinacho tokea upande wa kulia chini na moja kwa moja hashtag hizo zitacopiwa tayari kwa kuziweka kwenye post yako kwenye mtandao wa Instagram.

Kwa maelezo marahisi zaidi angalia video hapo juu kwa hatua na hatua jinsi ya kufanya hatua hizi kwa urahisi na haraka.

Tumia (AI) Artificial Intelligence Kupata Likes Nyingi Instagram

Kwa kutumia njia hii na kuhakikishia utaweza kuanza kuona like zikiongezeka kwenye post zako na utaweza kuwafikiwa watu wengi zaidi kwa haraka na kwa urahisi.

Kitu cha muhimu kumbuka unatakiwa kutumia hashtag ambazo hazizidi 15 na pia hakikisha unatumia hashtag tofauti kwenye kila picha ili kusaidia kufikia watu tofauti kila siku.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use