Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Haya Hapa Maujanja Usiyoyajua Kwenye Simu ya Android

Jaribu maujanja haya kwenye simu yako ya Android
Haya Hapa Maujanja Usiyoyajua Kwenye Simu ya Android Haya Hapa Maujanja Usiyoyajua Kwenye Simu ya Android

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anaye jua kila kitu, tena hasa kwenye ulimwengu huu wa teknolojia kuwa mjuzi wa kila kitu ni swala gumu sana kwani teknolojia inabadilika kila siku. Kuliona hili hivi leo nimekuletea maujanja ya android ambayo inawezekana ulikua hujui kuhusu kama yanawezekana kwenye simu yako.

Kumbuka baadhi ya maujanja haya yanawezekana yasifanikiwe kwenye baadhi ya simu za Android na kama hilo litakuwa ni moja ya tatizo ambalo utakutana nalo basi unaweza kutujuza kupitia sehemu ya maoni hapo chini na pengine tunaweza kutafuta ufumbuzi wote kwa pamoja, basi baada ya kusema hayo bila kupoteza muda twende tukangalie maujanja haya.

Advertisement

Game Inayopatikana Kwenye App ya Google

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia app ya Android basi ni lazima unaijua app ya Google, hapa sija maanisha app ya Google Chrome hapana, hapa nazungumzia app ya Google ambayo inakuja kwenye simu yako ikiwa na logo yenye alama ya “G” na mara nyingi hua kwenye folder moja na app mbalimbali za Google.

Sasa sijui kama ulikuwa unajua kua ndani ya app hiyo kuna Game ambayo unaweza kuicheza pale unapokuwa huna Internet, Game hiyo ni rahisi sana kuipata lakini kama hujui njia za kufuata huwezi kuipata. Sasa ili kupata game hiyo, zima kabisa Internet kwenye simu yako, kisha ingia kwenye app ya Google kisha andika chochote na kisha bofya kitufe cha kutafuta.

Baada ya hapo utaona Google ikiandika Mobile data off, kwa pembeni yake utaona duara lenye picha ya katuni na alama ya play kwa chini, bofya hapa kisha moja kwa mja utaanza kuona Game hiyo, ili kucheza unahitaji kubofya kwenye kioo chako kwaajili ya kukwepa ndege wanaopita kwa juu, kumbuka unapo bofya mara nyingi zaidi ndipo katuni huyo anavyozidi kwenda juu zaidi.

Haya Hapa Maujanja Usiyoyajua Kwenye Simu ya Android

Tumia Akaunti Mbili Kwenye Simu Moja Bila Programu Yoyote

Kwenye sehemu hii sina uhakika kama inawezekana kwenye kila simu hivyo unaweza kunijulisha hapo chini kama sehemu hii ipo kwenye simu yako. Lakini kwa upande wa Samsung sehemu hii inapatikana kwenye simu zenye mfumo wa Android kuanzia Android 7.0 (Nougat).

Sasa ili kupata sehemu hii ingia kwenye sehemu ya Settings kisha bofya sehemu ya Advanced features alafu bofya sehemu ya Dual Messenger. Kumbuka sehemu hii inafanya kazi kwenye baadhi ya Apps ambazo ni kama WhatsApps, Facebook, Messenger, Skype na nyingine kama hizo.

Haya Hapa Maujanja Usiyoyajua Kwenye Simu ya Android

Funga Application Kabisa Baada ya Kumaliza Kutumia

Kuna wakati unakuta unataka kutumia app mara moja tu kwa mfano app kama Play Store ambayo huwa na mtindo wa ku-update application bila hata ruhusa, njia hii inaweza kusaidia sana kuzima app hiyo mara baada ya kutumia. Pia njia hii inaweza kusaidia sana kutunza battery yako kwenye simu yako ya Android.

Unachotakiwa kufanya ingia kwenye simu yako kisha bofya sehemu ya Settings > About > Software Information kisha tafuta mahali palipo andikwa Build number, bofya hapa mara 5 mpaka utakapo letewa ujumbe kuwa sehemu ya developer imewashwa rasmi. Kumbuka menu zinatofautiana kwenye kila simu hivyo kitu cha msingi unatakiwa utafute About > Build number.

Haya Hapa Maujanja Usiyoyajua Kwenye Simu ya Android

 

Baada ya kuwasha sehemu hii rudi mpaka mwanzo wa Menu kuu ya Settings kisha utaona sehemu mpya inayoitwa Developer options ingia hapa kisha tafuta sehemu ya Don’t keep activities weka tiki kwenye sehemu hii na utakuwa umemaliza, sehemu hii itakusaidia sana lakini pia inaweza kuzuia notification kwenye baadhi ya apps ambazo umezoea zinakutumia notification kama vile WhatsApp na nyingine kama hizo.

Haya Hapa Maujanja Usiyoyajua Kwenye Simu ya Android

Badilisha App Moja na Nyingine kwa Haraka

Kama kwa namna yoyote imetokea unataka kubadilisha app moja na nyingine kwa haraka njia hii itakusaidia sana. Kwenye kubadilisha apps hapa na maana kama ulikuwa unatumia app moja na ukatoka kwenye app hiyo ukafungua nyingine, lakini baada ya muda kama unataka kurudi kwenye app ya awali badi unaweza kubofya kitufe cha box MARA MBILI kitufe ambacho kina kuwa upande wa kushoto au wa kulia kwenye baadhi ya simu za siku hizi.

Haya Hapa Maujanja Usiyoyajua Kwenye Simu ya Android

Na hayo ndio maujanja ya android ambayo pengine ulikuwa hujui kupitia simu yao, kwa maujanja zaidi pamoja na mambo mengine mbalimbali hakikisha una subscribe kwenye channel yetu ya Tanzania Tech hapa nakuahidi utapata maujanja mengi mbalimbali. Pia kwa maujanja zaidi kama haya, unaweza kusoma hapa kujua Menu za siri ambazo ulikuwa huzijui kwenye kompyuta ya Windows 10.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use