Namna ya Kufanya Smartphone Yako Ikae na Chaji Zaidi

Namna ya Kufanya Smartphone Yako Ikae na Chaji Zaidi Namna ya Kufanya Smartphone Yako Ikae na Chaji Zaidi

Watu wengi wanatumia smartphone siku hizi lakini ubora wa simu yako pamoja na ubora wa battery yako ndio kinachofanya smartphone yako iwe bora zaidi. Lakini kama unavyojua siku hizi simu nyingi smartphone hazikai na chaji kwa kiwango tunacho itaji, hata hivyo wingi wa application katika simu yako pamoja na ukubwa wa screen yako ni moja kati ya vitu vinavyofanya simu yako kutokukaa na chaji je unafanyaje ?. Kwa wanaume ninguu sana ku-beba “power bank” kila maahali tunapoenda hii inatokana na udogo wa mifuko pamoja na nguo tunazo vaa pia na aina ya mabegi tunayo beba, lakini kwa bahati nzuri dada zetu wanauwezo wa ku-beba “power bank” hii inatokana na kwamba wengi wao hubeba mikoba na si rahisi kumuona akiwa ameuwacha hata kama sehemu anayoenda nika karibu sana, kitu ambachao kwa wanaume wengi ni ngumu sana kukifanya, huwezi ukatembea na begi au ukaweka mfukoni simu pamoja na “power bank” kila mahali utakapo kwenda, hivyo basi kuwa na simu isiyokaa na chaji nitatizo kubwa sana hasa kwa wanaume japo kua hata kwa wanawake ni tatizo.

Zifuatazo ni njia za kusaidia smartphone yako kukaa na chaji njia hizi ni rahisi sana kufuata na zitasaidia simu yako kukaa na chaji kwa urahisi. Kuliko kuuza simu yako na kununua nyingine kisha ukute tatizo lipo palepale.

  1. Tumia “auto-brightness” – hii ni kwaajili ya screen ya simu yako kutokana na kwamba simu nyingi zenye vioo vikubwa zinatumia chaji nyingi. Hii usababishwa na sababu nyingi moja wapo ni kiasi cha mwanga unaotoka katika simu yako, ni vema kutumia “auto-brightness” kwani hii usaidia kupunguza kiasi cha mwanga pale ambapo hauitajiki kwenye simu yako. katika smartphone nyingi sehemu hii ya kupunguza mwanga upatikana kwenye “screen settings”.
  2. Ondoa matangazo kwenye simu yako – Mara nying kama unafanya installation ya application ni vema kusoma specification zake kwenye “Google Play Store”. Watu wengi kwa sasa utumia namna hii kujipatia kipato kwa kuweka matangazo kwenye application zao, hili linachangia sana katika umalizaji wa chaji katika simu yako kwani matangazo hayo hua yanaendelea kutokea hata kama utumiii simu yako. Jinsi ya kuondoa matangazo kwenye smartphone yako bonyeza hapa >> HAPA
  3. Hakikisha Email zako zinaingia kwa muda unaotaka – Mara nyingi ukisha nunu smartphone yako utakuta baada ya siku moja au masaa machache email inaingia kila baada ya muda mfupi pale utakapo tumiawa email inaingia moja kwa moja kwenye inbox yako, njia hii si nzuri sababu kila wakati simu yako inakua iki-“sync” na server za Google kila mara utumiwapo email. Kutumiaka kwa server hizo kila mara kuna sababisha simu yako kutumia chaji mara mbili ya ile ya kawaida hivyo kupelekea simu yako kutokukaa na chaji.
  4. Usisikilize mziki kwenye Internet – Techolojia ya sasa inakuwezesha kusikiliza mziki kwenye internet yani “ku-stream” bila kikomo kwa kutumia application kama vile “Dizzer” Mziki na nyingine nyingi, kila unapotumia application hizi au internet yenyewe kusikiliza mziki chaji yako inapungua kwa haraka zaidi kwani kama nilivyo eleza awali ni lazima simu yako itumie server za application hiyo au website uliyotembele ili uweze kusikiliza mziki, hivyo basi hii usababisha chaji yako kupungua kwa haraka kuliko kawaida.
  5. Hakikisha unazima wireless pamoja na Bluetooth kama huitumii – wengi wetu tunasahau kuzima baadhi ya vitu kwenye simu zetu baada ya kumaliza kutumia, wireless na bluetooth ni moja kati ya vitu vinavyo sahaulika sana na watu wengi sana kwa sasa, Bluetooth na wireless ni moja kati ya technolojia zinazo tumia mawimbi maalumi ku-unganisha kati ya kifaa kimoja na kingine au kifaa na internet mawimbi haya ili yeweze kusukumwa na kufikia kifaa kingine yanaitaji nguvu ya simu yako au battery hapo ndipo chaji unapotumiak kwa wingi kutokana na umbali na kiasi cha mawimbi kinacho tolewa na simu yako. Kumbuka kila simu inauwezo wake tofauti wa kusukuma mawimbi hayo.
  6. Kumbuka kuangalia application ipi inatumia chaj sana – Kwa wale watumiaji wa smartphone wanaojua kutukia simu hizo kwa undani lazima utakua umekutana na sehemu inasema “Battery Usage” ni vema kuangali sehemu hii kila saa kwani inasaidia kukwambia ni application ipi inatumia chaji sana ili kukupa nafasi ya wewe kuiondoa au kuizima application hiyo.

Kumbuka kama umefuata njia zote hizi na bado smartphone yako haikai na chaji usijali, unaweza uka download application ambazo kazi yake ni kusaidia smartphone yako kukaa na chaji zaidi na zaidi kila siku. Moja kati ya application hizo ni “DU Battery SaverDownload Hapa na “Batter DoctorDownload Hapa zote hizi zipo kwenye Google Play Store.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use