Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kufuta Kwa Haraka Picha na Mafaili Yanayofanana

Tumia njia hizi kuondoa picha zinazo jirudia kwenye simu yako
Jinsi ya Kufuta Kwa Haraka Picha na Mafaili Yanayofanana Jinsi ya Kufuta Kwa Haraka Picha na Mafaili Yanayofanana

Ni kweli kwamba kila mtu amewahi kupiga picha na kujikuta kuna picha nyingine zinazofanana, hii inatokea mara nyingi kama umeona picha ya kwanza haijatokea vizuri na hivyo ukalazimika kupiga icha nyingine mbili ama nne zinazofanana ili kuweza kupata picha moja unayo iyopenda zaidi.

Lakini kutoka na kufanya hivi mara nyingi simu inaweza kujaa haraka sana tena hasa kama wewe ni mpenzi wa kupiga picha kwenye simu yako, kuliona hili ndio maana leo nimekuletea njia rahisi na za haraka za kuweza kupata na kufuta picha zilizo jirudia kupitia simu yako ya Android.

Advertisement

Njia hizi ni rahisi sana na huna haja ya kupoteza muda mwingi bali unacho hitaji ni kufuata hatua hizi chache na moja kwa moja utaweza kuzipata picha zinazojirudia ikiwa pamoja na njia rahisi ya kuweza kufuta picha hizo kama unahitaji. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia hizi.

Remo Duplicate Photos Remover

Na uhakika kwa namna yoyote kama umeshawahi kutumia simu yako kupiga picha basi lazima unazo picha zilizo jirudia kwenye simu yako, App ya Remo Duplicate Photos Remover ni app rahisi sana kutumia na ambayo itakusaidia kuondoa picha zote zilizo jirudia hata kama simu yako imejaa picha, app hii ni ya bure na rahisi kutumia hivyo na uhakika utaweza kutumia kwa asilimia 100.

Download App Hapa

Duplicates Remover

Sasa kama wewe unazo picha pamoja na video zilizo jirudia kwenye simu yako basi app hii ni muhimu sana kuwa nayo, Duplicates Remover itakusaidia kuondoa picha pamoja na video zote zilizo jirudia kwa urahisi na haraka. Kama zilivyo app nyingine kwenye list hii app hii pia ni rahisi sana kutumia na uhakika utaweza kutumia kwa asilimia 110.

Duplicates Remover
Price: Free

Download App Hapa

Duplicate Files Fixer and Remover

Njia ya mwisho kwenye makala hii ni kwa kutuia app ya Duplicate Files Fixer and Remover, app hii ni nzuri sana na tofauti na app nyingine kwenye list hii, yenyewe inaweza kukusaidia kupata picha, mp3, video na mafile ya aina nyingine yaliojirudia. Kama unataka kuongeza nafasi ya simu yako basi nakushauri kutumia app hii angalau mara moja kila mwezi na utakuja kuniambia kwenye maoni hapo chini kuhusu ubora wa app hii. Kama app nyingine app hii ni rahisi sana kutumia.

Download App Hapa

Na hizo ndio njia ambazo unaweza kutumia kuweza kupata picha zilizo jirudia kwenye simu yako ya Android. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kurudisha picha zilizo futika kwenye simu yako ya Android.

Kwa habari zaidi na maujanja hakikisha una subscriber kwenye channel yetu hapa, kwani tunaenda kujifunza maujanja mbalimbali ambayo yanaweza kurahisisha maisha yako hasa kwenye utumiaji wa simu, kompyuta na teknolojia kwa ujumla.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use