Opera Yaja na Aina Mpya ya Kivinjari cha Opera Touch

Kivinjari hichi kitakuwezesha kukitumia kwa mkono mmoja
Opera Touch Opera Touch

Kampuni ya Opera ambayo ndio watengenezaji wa kivinjari maarufu cha Opera Mini pamoja na programu ya Opera Max ambayo sasa imenunuliwa na Samsung. Hivi leo opera wametangaza kuja na aina mpya ya kivinjari cha Opera Touch, Kivinjari hicho kitakuwa kinapatikana kwenye mifumo yote ya Kompyuta, Android pamoja na iOS.

Kwa mujibu wa Opera, kwa upande wa simu kivinjari cha Opera Touch kimetengenezwa maalum kwaajili ya kuweza kutumika kwa mkono mmoja huku kikiwa na sehemu mpya mbalimbali kama vile sehemu yenye kukupa uwezo wa kushiriki tovuti uliyotembele kwenye simu kwenda kwenye kompyuta au kinyume.

Advertisement

Kivinjari hicho kitakupa uwezo wa kutembelea tovuti mbalimbali kwa kutumia mkono mmoja kwa kubofya huku unashikilia kitufe maalum kinacho tokea katikati ya kivinjari hicho.

Kwa sasa kivinjari hichi kipya cha Opera Touch kinapatikana kwenye mfumo wa Android pekee na inasemekana kitakuja kwenye mifumo mingine siku za karibuni, Unaweza kupakua kivinjari hicho kwa kubofya hapo chini.

Opera Touch – Android

Opera Touch
Price: Free

Baada ya kupakua kivinjari hichi kwenye simu yako ya Android, tuambie kwenye maoni hapo chini unaonaje kivinjari hicho kipya kutoka kwa Opera.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use