Apps# 9 Hizi Hapa App Nzuri za Kupima Uwezo wa Simu Yoyote

Kama unataka kujua uwezo halisi wa simu yako, pakua app hizi nzuri
App za kupima uwezo wa simu App za kupima uwezo wa simu

Kuna programu nyingi sana Play Store na App Store, programu hizo zina uwezo wa kufanya mambo mbalimbali kwenye simu za iPhone na Android, iwe unataka kufanya mambo makubwa au hata mambo madogo ya kawaida, masoko haya yanayo programu au Apps nyingi nzuri ambazo zinaweza kukusaidia wewe kufanya mambo hayo.

Sasa wiki hii nina kuletea Apps ambazo zitakusaidia wewe kuweza kufanya majaribio au kupima uwezo wa simu yako na kuweza kukupa matokeo ambayo utaweza kujua ubora wa kila kifaa kilichoko ndani ya simu yako. App hizi pia zitaweza kukusaidia zaidi endapo unataka kununua simu iliyo tumika, au simu ambayo unadhani kwa namna moja ama nyingine sio simu halisi (simu feki).

Apps hizi pia zitakusaidia kuweza kujua matatizo madogo madogo ndani ya simu yako hivyo kurahisisha kuweza kujua hatua za kuchukua mapema kabla ya tatizo hilo kuwa kubwa. Sasa bila kupoteza muda, twende tuka angalie apps hizi nzuri.

Advertisement

1. TestM

  • Android 
TestM
Price: Free
  • iOS

App hii itakusaidia kuweza kufanya majaribio ya kila kitu kwenye simu yako ikiwa pamoja na kukupa ripoti makini ya majaribio hayo, uzuri ni kuwa app hii haina matangazo hivyo haina usumbufu na ni rahisi kutumia. Muhimu ni kwamba unatakiwa kufuata hatua zote kwa usahihi ili uweze kupata ripoti kamili na yenye uhakika. Kama unatumia iOS unaweza kupakua app hii pia.

2. Geekbench 4

  • Android
Geekbench 4
Price: Free
  • iOS
Geekbench 4
Price: $0.99

Geekbench 4 ni moja ya App ambazo hizi ni muhimu kwa wale wanaotka kujua uwezo wa Processor ya simu fulani, App hii itakusaidia kupima uwezo wa processor yako pamoja na nguvu na uwezo wa battery ya simu yako, App hii pia inasaidia sana kama unaona simu yako imekuwa (Slow) App hii itakusaidia kujua kama tatizo liko kwenye simu yako ama lah!. App hii inapatikana pia kwenye mfumo wa iOS, lakini itakubidi kulipia Tsh 2,500 ili kupakua.

3. AnTuTu Benchmark

  • Android
AnTuTu Benchmark
Price: Free
  • iOS
‎AnTuTu Benchmark
Price: Free

Antutu ni App nyingine bora sana ya kupima uwezo wa simu yako, App hii itakusaidia kuweza kujua mambo mbalimbali kwenye simu yako ikiwa pamoja na uwezo wa simu yako kucheza game zenye uwezo mkubwa, uwezo wa RAM ya simu yako pamoja na mambo mengine mbalimbali. App hii ni nzuri sana na inafanya majaribio kwa undani na kukupa ripoti yenye uhakika.

Na hizo ndio Apps ambazo nimekuandalia kwa siku ya leo, kama ulipitwa na App za wiki iliyopita unaweza kusoma apps hizo hapa. Kwa maoni au ushauri tuandikie kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

5 comments
  1. kwanza hongereni sana nafurahi kutumia app ya ndugu zetu ila nina swali samahan kama nitakuwa nje ya topic nauliza hivi mnahusika na kutengeneza simu pia

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use