Instagram Yaondoa Kitufe cha IGTV kwenye Ukurasa wa Home

Sehemu hiyo sasa imehamishiwa kwenye ukurasa wa Explore
Instagram Yaondoa Kitufe cha IGTV kwenye Ukurasa wa Home Instagram Yaondoa Kitufe cha IGTV kwenye Ukurasa wa Home

Kama wewe ni mtumiaji wa sehemu ya IGTV kupitia app ya instagram basi inawezekana tayari umeona kwa sasa ni vigumu kuweka au kupost video mpya ya IGTV kupitia app ya Instagram, hii ni kwa sababu Instagram imeondoa kitufe cha IGTV kupitia app ya Instagram.

“Tunapoendelea kufanya kazi ili kuifanya iwe rahisi kwa watu kuunda na kugundua yaliyomo kwenye IGTV, tumejifunza kuwa watu wengi wanapata yaliyomo kwenye IGTV kupitia preview Feed, channel ya IGTV, kupitia app ya IGTV, pamoja na kupitia profile mbalimbali. Ni wachache sana wanaobofya kwenye ikoni ya IGTV kwenye kona ya juu ya kulia ya skrini ya nyumbani kwenye programu ya Instagram ” msemaji wa kampuni ya Facebook aliambia tovuti ya TechCrunch.

“Sisi kila wakati tunakusudia kufanya app za Instagram kuwa rahisi kutumia iwezekanavyo, kwa hivyo kwa sasa tunaondoa ikoni (Icon ya IGTV) hii kulingana na maoni kutoka kwa watumiaji wetu.”

Advertisement

Instagram Yaondoa Kitufe cha IGTV kwenye Ukurasa wa Home

Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji huyo, watumiaji wa instagram watakuwa hawaitaji app ya IGTV kama wanataka kuangalia video mbalimbali za IGTV kwani zitakuwa zinaonekana kwenye profile za watumiaji, kupitia Tab ya Explore, pamoja na kupitia kwenye home feed.

Kwa wale ambao wanataka kuweka video za IGTV sasa inabidi kupitia sehemu ya Explore ambapo utaona kitufe cha IGTV upande wa kushoto juu, ambapo baada ya kubofya hapo utaweza kuona video za IGTV pamoja na sehemu ya kuweka video ambayo ipo juu upande wa kulia kwenye ukurasa huo wa IGTV.

Instagram Yaondoa Kitufe cha IGTV kwenye Ukurasa wa Home

Kwa mujibu wa tovuti ya social media examiner, hadi kufikia septembar mwaka jana 2019, IGTV ilikuwa imechukua asilimia 9 tu kwenye mitandao inayotumiwa na watu zaidi kwa upande wa video, huku mtandao wa YouTube ukiwa unaongoza kwa kuchukua asilimia 57 ya mitandao yote.

Instagram Yaondoa Kitufe cha IGTV kwenye Ukurasa wa Home

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use