Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

HP Yazindua Laptop/Tablet Mpya ya HP ZBook x2

Laptop/Tablet hii ni kimbilio la Graphics Designers wote
Laptop/Tablet Mpya ya HP ZBook x2 Laptop/Tablet Mpya ya HP ZBook x2

HP ni kampuni ya siku nyingi sana kwenye ulimwengu mzima wa utengenezaji wa kompyuta bora, ndio maana sio ajabu kuona kampuni hii ikitoa laptop au kompyuta mpakato zenye nguvu na uwezo wa hali ya juu sana.

Hivi leo kampuni hiyo imetangaza rasmi ujio wa kompyuta yake mpya ambayo inauwezo wa kuwa laptop na tablet yaani 2 in 1. Laptop hiyo ya HP ZBook x2 ina uwezo mkubwa sana huku ikiwa imetengenezwa maalum kwa wale watumiaji wa programu za Adobe pamoja na wabunifu wa michoro kupitia kompyuta yaani Graphics Designers.

Advertisement

Laptop hii imetengenezwa kwa processor ya Intel Core i7 (Kaby Lake) processor yenye uwezo wa 4.2GHz Turbo ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 32 huku ikiwa na GPU ya Nvidia Quadro M620 ambayo inaweza kuendesha programu zako za Adobe na Autodesk Design Suite kwa haraka.

Haija ishia hapo HP ZBook x2 inakuja na kioo cha inch 4 chenye teknolojia ya anti-glare touch screen huku kikiwa na uwezo wa kuonyesha vizuri video za 4K. Kwa upande wa USB laptop hii inayo Thunderbolt 3 USB 3.0 port ikiwa na sehemu ya chaji pamoja na HDMI 1.4 connector.

Kwa upande wa chaji laptop hii inasemekana kukaa na chaji hadi masaa 10 huku ikiwa na teknolojia ya Fast Charging ambayo inauwezo wa kuchaji Laptop hiyo kwa asilimia 50 kwa dakika 30 tu. HP ZBook x2 imetengenezwa kwa makava maalumu yenye Aluminum pamoja na Magnesium.

Laptop hii pia inakuja na teknolojia mbalimbali za ulinzi ikiwemo fingerprint reader, facial recognition, TPM 2.0  pamoja na HP Sure Start Gen311 ambayo kazi yake ni kulinda mfumo wa BIOS. Laptop hii inategemewa kuingia sokoni mwezi wa kumi na mbili huku ikiwa na Price tag ya dollar $2,730 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 6,200,000 (bei inaweza kuongezeka kwa Tanzania).

Je umeonaje sifa na muundo wa laptop hii.? tuambie kwenye maoni hapo chini, Kwa habari zaidi za Teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya kwa upande wa teknolojia, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa haraka zaidi.

Chanzo : CNET

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use