Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kama Umenunua Laptop Mpya ya HP Miaka 2 Iliyopita Soma Hii

Muhimu kama unatumia HP, baadhi ya laptop zina matatizo ya Battery
Hp Laptop Hp Laptop

Kampuni ya HP kupitia mitandao mbalimbali imewatangazia wateja wake ambao wamenunua baadhi ya laptop nchini Canada na baadhi ya nchi kuwa, imegundua kuwepo na ubovu wa baadhi ya laptop hizo kwa upande wa battery.

Kampuni hiyo pia imesema imepokea baadhi ya ripoti kuhusu kuyeyuka na kuwaka moto kwa baadhi ya battery za laptop zilizo nunuliwa kati ya kipindi cha mwezi December 2015 hadi December 2017. Hata hivyo kampuni hiyo kwenye ukurasa wake maalum inasema kuwa laptop hizo zaidi ya 50,000 kati yake laptop 2,600 ziliuzwa nchini Canada.

Advertisement

HP imetangaza kuwa inawataka wateja wake wote walio nunua laptop, pamoja na mobile workstation computer kati ya kipindi hicho kuhakikisha kuwa wanawasha sehemu maalum ya kuzuia kuharibika kwa battery inayoitwa “battery safety mode” ambayo itakuja kwenye update za Bios za laptop ambazo zimetajwa kuwa na tatizo hilo.

Hata hivyo kampuni hiyo imetoa list ya laptop ambazo zinauwezekano wa kuadhiriwa na tatizo hilo na hivyo kuitajika kubadlishiwa battery ili kuepusha matatizo hayo yanayoweza kutokana na battery zilizopo sasa.

HP imehitaji watu kuchukua hatua za haraka kwa kuangalia battery zao kwa kutumia programu maalum inayopatikana HAPA na kama laptop yako ina tatizo hilo basi update sehemu ya Bios na washa sehemu ya “Batter Safety Mode” kama ilivyo elekezwa kwenye ukurasa HUU.

Kwa taarifa zaidi kuhusu hili unaweza kutembelea Ukurasa maalum wa HP Hapa na utapata maelekezo zaidi nini cha kufanya kama laptop yako imeadhiriwa na tataizo hili.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use