Jinsi ya Ku-install Windows 10, 8, 7 na XP Kwenye Simu ya Android

Kama unataka kuweka Windows kwenye simu yako basi fuata hatua hizi
windows kwenye android (1) windows kwenye android (1)

Kutokana na teknolojia kubadilika sana vile vile hata simu zetu nazo zimekua zikibadilika kila siku, simu zetu zimekuwa zimebadilika kuanzia uwezo, vitu inavyofanya mpaka matumizi ya simu hizo. kuelewa mabadiliko hayo leo Tanzania Tech tunaenda kukuonyesha njia rahisi ya kuinstall Windows 7, Windows 8, Windows 10 pamoja na Windows XP kwenye simu yako ya Android.

Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa uwezo wa kutumia Windows kwenye simu yako unaweza kukusaidia wewe kutumia simu yako kama kompyuta, njia hii itakusaidia sana kama simu yako inauwezo wa kutumika kwenye screen kubwa ili kukupa uwezo wa kufanya vitu mbalimbali kama unavyo tumia kwenye kompyuta, yaani bila tofauti kubwa utafauti ni kwenye graphics pekee.

Kwa kuanza unatakiwa kuwa na simu yako ya Android yenye RAM at-list GB 1 na kuendelea, uharaka wa kuinstall Windows kwenye simu yako unategemeana sana na Uwezo wa RAM ya simu yako. Basi baada ya kuhakikisha una simu yenye uwezo huo basi moja kwa moja ingia kwenye soko la Play Store kisha tafuta App inayoitwa Limbo PC Emulator QEMU ARM x86 (unaweza kudownload kwa kubofya hapo chini).

Advertisement

UPDATE 2020 : Programu ya Limbo sasa haipo tena kwenye soko la Play Store ila bado unaweza kutumia njia hii kwa kudownload programu hii kupitia link hapo chini.

Download Limbo APK

Baada ya kuinstall programu hiyo kwenye simu yako basi endelea moja kwa moja kwa kudownload Windows unayotaka kuinstall kwenye simu yako, chagua link ya aina ya windows unayotaka kwa kusoma jina lake.

UPDATE : Link zote sasa zinafanya kazi vizuri kabisa

Baada ya hapo endelea kwa kuingia kwenye programu yako ya File Manager kisha tafuta folder lenye jina la Limbo, baada ya kupata Folder hilo rudi kwenye programu yako ya Windows kisha copy file lako ambalo uli download hapo awali kumbuka file hilo linakuwa na format ya .IMG baada ya ku-copy paste kwenye folder la Limbo kisha washa programu yako ya limbo ulio download hapo mwanzo na kwa umakini fuata hatua hizi.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

40 comments
  1. Hakikisha una una unzip file maana liko kwenye zip file kisha extraxct kwenye simu yako unaweza kutumia programu yoyote ya ku unzip kama huna tafuta play store au app store.

 1. Maoni*aiseee wakuu hizo link za Windows km zimeixha time 2badilishien coz na install kweny cm ya tecno y4 zinakataa

   1. Sawaaa sasa nime download hiyo window 8.1 lakini haijaingia katika mfumo wa .IMG bali ipo hivi .ISO
    Kwa maelekezo uliyo weka inagoma.

 2. Sawaaa sasa nime download hiyo window 8.1 lakini haijaingia katika mfumo wa .IMG bali ipo hivi .ISO
  Kwa maelekezo uliyo weka inagoma.
  Msaada hapo

 3. Maoni*aiseee mkuu nimedonload xp kweny cm ya tecno y4 lakn baada ya installing nikafany km maelezo yalivo lakn katk process inaniandikia no botable device so mkuu naomba solutions

 4. Maoni**Abdul *ni hivi mkuu nikiingiza hizo process inaniandikia press volume shoot down nkishusha voliom inAanza kuandika maneno mengi alaf mwish inaandika no botable device inaendelea hivo nimeiacha kwa dakika 40 inaendelea kutafta

 5. Ukiifungua hiya App ya kuna badhi ya features hazionekani (Tecno C8), mfano user interface ili nichague SDL. n.k
  Tatizo ni nini??

 6. Mbona nadownload window znagoma? Yaan wananiletea picha ila kuisevu no shida, nisaidieni tafadhali

 7. Katika kudownload Windows imenidirect kutumia MEGA app but nikiclick link inanipeleka MEGA app then haipakui file.shida ni nini?

 8. Ndug mtaalam mm sim yang ni Tecno Y3+ ,napenda sana hii huduma ya kueweka window kweny cm lakn nimefel sasa cjui tatzo ni nn? Au simu cm haisapot maana nmejaribu window zote na ninaacha kwa muda usiopungua lisaa lakn matokeo bado ni hasi.Naomba nielekeze mkuu tafdhali.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use