Rudisha Mafile Yaliyofutika Kwenye Kompyuta, Simu na Flash

Njia hii ni bora na rahisi kutumia kwa mtu yoyote anataka kurudisha mafile yaliyopotea
Rudisha Mafile Yaliyofutika Kwenye Kompyuta, Simu na Flash Rudisha Mafile Yaliyofutika Kwenye Kompyuta, Simu na Flash

Ni wazi kuwa hakuna mtumiaji wa vifaa vya kielektroniki kama kompyuta, simu au USB flash ambaye hajawahi kupoteza au kufuta kitu kwa bahati mbaya na baadae kuhitaji kurudisha kitu hicho.

Najua nilishawahi kuongelea njia nyingine za kurudisha vitu vilivyo futika kwenye simu yako, lakini njia hii ni njia ya tofauti na ambayo pengine inaweza kuchagia kupata vitu vyako vilivyo futika.

Kwa kuanza ni muhimu kujua kuwa unaweza kurudisha vitu kwenye simu, USB Flash na kompyuta zote yenye mfumo wa Windows, pamoja na Mac. Njia hizi nitakazo zionyesha hapa ni njia bora na zinafanya kazi bure kabisa. Kitu cha muhimu hakikisha unasoma makala hii hadi mwisho.

Advertisement

Basi baada ya kusema hayo, moja kwa moja kwenye kompyuta yako ambayo imepoteza vitu pakua programu ya Wondershare Recoverit hapo chini. Pakua programu kulingana na aina ya kompyuta unayo tumia yaani Windows au MacOS.

Pakua Wondershare Recoverit Hapa

Programu hiyo ni toleo la bure na kupitia programu hiyo utaweza kurudisha vitu kwenye USB Flash, SD Card, Hard disk na hata kwenye kompyuta yako.

Rudisha Mafile Yaliyofutika Kwenye Kompyuta, Simu na Flash

Baada ya kudownload file husika hapo juu fungua file hilo kisha install programu hiyo kwenye kompyuta yako. Baada ya kuinstall vizuri kwenye kompyuta yako moja kwa moja chagua file njia ambayo unataka kutumia kurudisha vitu vyako vilivyopotea.

Unaweza kutumia menu kama inavyo onekana kwenye mfano hapo chini, na moja kwa moja subiri programu hii imalize kuscan na moja kwa moja utaweza kuona mafile yako yaliyofutika na utaweza kurudisha moja kwa moja kwa kutumia programu hii.

Rudisha Mafile Yaliyofutika Kwenye Kompyuta, Simu na Flash

Kama nilivyo kwambia, programu hii inaweza kurudisha mafile kupitia Kompyuta, USB Flash, external hard disk pamoja na vifaa vingine mbalimbali. Kama unataka kurudisha mafile yaliyopote kwenye simu yako basi unaweza kutumia programu Dr Fone hapo chini.

Kama ilivyo programu hapo juu, programu ya Dr fone nayo ni programu kutoka wondershare, programu hii pia inakupa uwezo mkubwa wa kurudisha mafile yaliyopote na utaweza kufanya hivyo kwa kutumia kompyuta yako.

Kwa kuanza hakikisha unapakua programu kupitia link hapo chini, kisha baada ya hapo install vizuri kwenye kompyuta yako. Baada ya kuinstall moja kwa moja hakikisha simu yako ipo rooted, kama hujui kuroot simu unaweza kusoma makala hii hapa.

Pakua Dr Fone Hapa

Baada ya hapo chomeka simu yako kisha moja kwa moja bofya sehemu ya Data recovery kwenye programu hiyo ya Dr Fone.

Rudisha Mafile Yaliyofutika Kwenye Kompyuta, Simu na Flash

Baada ya hapo subiri baada ya muda programu hii iweze kuscan simu yako na moja kwa moja utaweza kuona mafile yako na utaweza kurudisha moja kwa moja kwenye simu yako au kusave kwenye kompyuta yako.

Kwa kufuata hatua hizo utaweza kurudisha mafile yako yaliyopotea kwenye kmpyuta, simu na USB flash. Kama unataka kujifunza njia zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kufufua USB flash drive iliyokufa kwa urahisi. Pia unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kufufua memory card iliyokufa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use