Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android

Hizi hapa hatua kwa hatua jinsi ya kuinstall Windows kwenye PC kwa kutumia Simu
Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android

Wote tunajua kuwa ili uweze ku-install windows kwenye kompyuta yako basi ni lazima uwe na USB Flash disk (Thumb Drive) au uwe na DVD yenye mfumo huo wa Windows.

Lakini ni wazi kuwa kadri siku zinavyokwenda kompyuta zenye sehemu ya kuweka CD zinazidi kupotea hivyo ni wazi kuwa lazima wote sasa tuanze kuzoea kuinstall Windows kupitia USB.

Lakini inakuaje kama huna Flash Drive au External..? Kuliona hilo leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia Kuinstall Windows kwenye kompyuta yako kwa kutumia simu yako ya Android. Njia hii ni rahisi na mtu yoyote anaweza kufanya kwa kufuata hatua hizi.

Advertisement

Mahitaji ya Muhimu

Kabla ya kuanza ni muhimu kujua kuwa ili kusudi uweze kuinstall Windows kwa kutumia simu yako ya Android ni lazima simu yako ya Android iwe na Uhifadhi angalau GB 5 au zaidi hakikisha hii sio uhifadhi wa Memory Card bali hakikisha ni uhifadhi wa ndani wa Simu (Internal Memory au ROM).

Pia hakikisha simu yako ipo Rooted, pia unatakiwa kuwa na waya wa simu yako unao onyesha data kwenye kompyuta, bila kusahau file la Windows unayotaka ku-install. Kama unataka kujua jinsi ya ku-root simu yako basi unaweza kusoma hapa.

Jinsi ya Kuinstall Windows kwa Kutumia Android

Kama simu yako ipo rooted basi moja kwa moja unaweza kuendelea kwenye hatua hizi. Ingia kwenye soko la Play Store kisha pakua app ya Drivedroid, unaweza kuinstall kwa kupitia link hapo chini.

DriveDroid
Price: Free

Baada ya kuinstall app hiyo, moja kwa moja fungua app hiyo na bofya sehemu ya Setup iliyopo chini upande wa kulia.

Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android

Baada ya hapo moja kwa moja app hii itahitaji Root Access, bofya sehemu ya ‘Acquire root’ ambayo inatokea katika ya app hiyo.

Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android

Baada ya hapo moja kwa moja sasa unaweza kuendelea kwa kuchomeka simu yako kwenye kompyuta na baada ya hapo bofya sehemu ya ‘Standard Android Kernel’ ndani ya app hiyo.

Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android

Baada ya hapo kama umefanya kila kitu kama nilivyo elekeza hapo juu basi utaweza kuona simu yako imeonekana kama USB drive kwenye kompyuta yako.

Kumbuka : Kama simu yako haita onekana kwenye kompyuta yako basi moja kwa moja rudi kwenye hatua iliyopita na chagua aina nyingine ya USB System kama inavyo onekana hapo juu.

Baada ya hapo moja kwa moja tuma file lako la Windows lenye format ya ISO kwenye USB Drive ya simu yako iliyotokea baada ya kufanya hatua zilizopita. Hakikisha muda wote simu yako inatakiwa kuungwanishwa na kompyuta.

Baada ya hapo unaweza kuendelea kwa kuchukua simu yako kisha fungua app ya Drivedroid na kisha bofya sehemu ya katika yenye alama ya jumlisha na kisha bofya ‘Add an image from file’.

Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android

Baada ya hapo unatakiwa kutafuta file la Windows lenye format ya ISO ambalo ulituma kwenye simu yako kwenye hatua iliyopita. Baada ya kupata lichague kisha bofya alama ya tiki iliyopo juu.

Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android

Baada ya hapo moja kwa moja chagua hosting option, kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android

Baada ya hapo utakuwa umemaliza na sasa unaweza kurestart kompyuta yako na kuchagua jina la USB ambalo linatumika kwenye simu yako na moja kwa moja utaweza kuinstall windows kwa kutumia simu yako.

Jinsi ya Kuinstall Windows Kwa Kutumia Simu ya Android

Kama unataka unaweza kusoma hapa jinsi ya kuinstall Windows kwa kutumia Flash Drive au pia unaweza kusoma hapa jinsi ya kuinstall Windows hatua kwa hatua.

Kama kuna mahali umekwama unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use