Instagram Inategemea Kuanza Kuficha Idadi ya Like Kwenye Picha

Sasa hutoweza kuona idadi ya likes kwenye picha ya mtu mwingine
Instagram Inategemea Kuanza Kuficha Idadi ya Like Kwenye Picha Instagram Inategemea Kuanza Kuficha Idadi ya Like Kwenye Picha

Hivi karibuni watumiaji wengi wa mtandao wa Instagram wamekuwa wakiangalia zaidi, likes na followers na kusahau mambo mengine ya msingi. Kama ilivyosemekana awali instagram inategemea kubadilisha hili kwa kufanya mabadiliko ya muonekano kwenye apps zake.

Mabadiliko makubwa yanayo tegemewa kufanyika ni pamoja na mabadiliko ya jinsi muonekano mzima wa profile utakavyokuwa, unaweza kusoma hapa kujua zaidi kuhusu mabadiliko hayo na mengine mengi.

Sasa tofauti na mabadiliko ya profile, mabadiliko mengine ambayo yanasemekana kuwa kwenye hatua ya majaribio ya ndani kwa sasa ni pamoja na majaribio ya sehemu inayo onyesha idadi ya likes kwenye picha. Sehemu hii inasemekana kuondolewa kabisa na sasa hutoweza kuona idadi ya likes kwenye picha ambazo sio za kwako. Inasemekana kuwa kama picha iko kwenye profile yako basi ndipo utaweza kuona idadi ya like lakini kama sio ya kwako hutoweza kuona sehemu hiyo ambayo huonyesha idadi ya likes kwa namba.

Advertisement

Instagram Inategemea Kuanza Kuficha Idadi ya Like Kwenye Picha

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu hata kama picha ni yako hutoweza kuona idadi ya likes moja kwa moja kwenye picha husika bali sasa utaona idadi ya likes kwenye ukurasa mwingine kama unavyoweza kuona kwenye picha ya katikati.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya The verge ambayo iliongea na msemaji wa instagram kutaka kujua kuhusu mabadiliko hayo, msemaji huyo alisema kuwa sehemu hii bado haipo kwenye majaribio ya jumla kwa sasa ila Instargram imekuwa ikiangalia njia mbalimbali za kupunguza motisha kwa watumiaji wa instagram na kuwataka kupost zaidi vitu kwa ajili ya kuunganisha jamii.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za lini sehemu hii itakuja rasmi kwenye apps za instagram, lakini kama unavyoweza kuona instagram sasa inakuja na njia ya kuweza kuonda daraja la watu maarufu na watu wa kawaida kwenye mtandao huo na kuangalia zaidi nani anapost kitu gani kuliko kuangalia zaidi idadi ya followers pamoja na likes.

Kujua zaidi kuhusu sehemu hii pale itakapofika kwenye apps za Instagram hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kwani tutakupa habari zote kuhusu sehemu hii pindi tutakapo zipata.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use