F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Haya hapa mabadiliko yaliyo tangazwa kwenye mkutano wa F8 2019
F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Mkutano wa F8 2019 umeanza rasmi hapo jana na tayari mambo ya muhimu kwenye mkutano huo yamesha tangazwa rasmi. Kupitia makala hii tutaenda kuangalia mambo yote hayo kwa undani ikiwa pamoja na mabadiliko yote yaliyo tangazwa kuja kwenye mitandao ya Facebook, WhatsApp na Instagram.

Nini maana ya F8

Kwa kuanza labda tuzungumzie kidogo mkutano wa F8, Mkutano wa F8 ni mkutano ambao unahusisha wabunifu na watumiaji mbalimbali wa huduma za Facebook, Mkutano huu hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa tano ambapo kupitia mkutano huo Facebook hupata nafasi ya kuonyesha sehemu mpya zinazokuja kwenye huduma zake ikiwa pamoja na mambo mapya ya muhimu kwa upande wa wabunifu wa programu ambao hutumia huduma za Facebook.

Kwenye mkutano wa F8 mwaka huu, Facebook imeangalia zaidi kwenye (Privacy) faragha, mbali na hayo pia Facebook imetangaza ujio wa muonekano mpya wa tovuti ya Facebook, pamoja na app zake zote za mifumo ya Android na iOS. Mbali na hayo pia Instagram imeongezewa sehemu mpya pamoja na maboresho mengine ya App ya WhatsApp na WhatsApp Business, bila kusahau maboresho ya app ya kuchati ya Facebook Messenger.

Advertisement

Maboresho ya Facebook

Kwa kuanza labda tuanze na maboresho mapya ya Facebook, Facebook inakuja na muonekano mpya kabisa kwenye tovuti yake pamoja na app yake huku muonekano huo ukisemekana kuwa bora zaidi na unaofanyakazi kwa haraka.

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Muonekano huo unasemekana kuwa tofauti kabisa huku ukizingatia zaidi magroup pamoja na matamasha (Event) ndani ya tovuti hiyo ya Facebook. Kwenye muonekano huo mpya facebook inatarajia kuonyesha zaidi magroup na even kutoka mahali ulipo kwenye sehemu ya Feeds zaidi kuliko kuonyesha update kutoka kwa watu binafsi mara kwa mara.

Mbali na hayo, Facebook pia inakuja na sehemu mpya ya kuunganisha marafiki kwa urahisi zaidi sehemu ambayo itakuwa inaitwa Meet New Friends. Sehemu hiyo inasemekana kuunganisha marafiki kwa kuangalia shule mlizosoma pamoja au vitu vingine ambavyo huenda vinafanana.

Pia app za Facebook zimefanyiwa mabadiliko na zinakuja na mtindo mpya ambao unafanya kazi kwa haraka kuliko mtindo ule wa awali.

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Muonekano mpya wa Programu za Facebook kwa upande wa Android pamoja na iOS, Kama unavyoweza kuona mabadiliko kwenye ukurasa wa kwanza wa feed kama picha ya juu hapo inavyo onyesha.

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Kwa sasa muonekano huu unapatikana kwa nchi za Canada na USA na utakuja baada kwa nchi nyingine, unatakiwa kuhakikisha una update app yako ya Facebook ili kupata muonekano huo.

Mabadiliko ya Facebook Messenger

Kwa upande wa Facebook Messenger napo pia kuna mabadiliko ambayo yanategemewa kuja hivi karibuni, mabadiliko hayo yana angalia zaidi kwenye marafiki wa karibu na itamuwezesha mtumiaji kutumia chat na watu wa karibu.

Hayo yote yana wezeshwa na sehemu mpya ambayo utakuwa una uwezo wa kuweka picha na video zako za stories, kuchati na marafiki wa karibu pamoja na kutumiana picha na watu wako wa karibu.

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Mbali na hayo Facebook Messenger inakuja na programu maalum za kompyuta ambazo unaweza kutumia kwenye kompyuta yako bila kuwasha kivinjari chako kama ilivyo sasa.

Mabadiliko ya Instagram

Kwa upande wa Instagram, mabadiliko mapya ambayo yametangazwa ni pamoja na sehemu ya “Create Mode,” sehemu hii mpya itakupa uwezo wa kupost picha na video zako kwa urahisi ikiwa pamoja na sehemu mpya ambayo itakuruhusu kupost maneno ya kawaida yenye rangi kwa nyuma kama ilivyo kwenye mtandao wa Facebook.

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Mbali na hayo, Instagram imetangaza kuendelea kuleta sehemu ya kuruhusu watumiaji wachache kupost stika ambazo unaweza kuweka bidhaa na pale mtu anapo bofya hupelekwa kwenye ukurasa wa kununua bidhaa hiyo moja kwa moja. Sehemu hii itakuja kwa watu maarufu kwanza na baadae itaendelea kuwafikiwa watu wengine taratibu.

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Mtumiaji wa sehemu hiyo ataweza kupokea malipo moja kwa moja kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa urahisi na haraka.

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Kitu kingine ambacho kimetangazwa kwenye mkutano huo ni pamoja na sehemu ya kuficha idadi ya like ambayo imetangazwa kufanyiwa majaribio nchini Canada na endapo majaribio hayo yaki fanikiwa basi sehemu hiyo inaweza kutoka rasmi kwa watumiaji wote.

Mbali na yote Instagram pia inakuja na stika za kuruhusu kupokea michango kwa urahisi kupitia mtandao huo. Mtumiaji ataweza kupokea michango kwa kuchagua stika ya Donation wakati unaweka picha au video kupitia sehemu ya Stories.

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Mabadiliko Mapya WhatsApp

Kwa upande wa WhatsApp hakuna mabadiliko makubwa sana zaidi ya uwezo mpya wa kuweka list ya bidhaa kupitia programu ya WhatsApp ya biashara

F8 2019 : Mabadiliko Mpya ya Facebook, WhatsApp na Instagram

Na hayo ndio mabadiliko muhimu ambayo nimeona nikujuze ambayo yametangazwa hapo jana kwenye mkutano wa F8 2019, Bado kuna sehemu nyingine ndogo ndogo ambazo hatuja zigusia kwenye makala hii hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use