Kwanini Infinix Note 30 ni Simu Bora Kuliko Galaxy A24

Kwanini wapenzi wa Infinix Note 30 wanaipenda zaidi kuliko Galaxy A24
Kwanini Infinix Note 30 ni Simu Bora Kuliko Galaxy A24 Kwanini Infinix Note 30 ni Simu Bora Kuliko Galaxy A24

Infinix NOTE 30 na Samsung A24 ni miongoni mwa simu janja ambazo zimeachiliwa Mwaka huu na kuuzika katika mataifa mbalimbali. Simu hizi zinatofautiana bei na baadhi ya sifa hivyo basi leo tutaangaza tofauti kati ya simu hizi mbili kwa kuangalia kipengele cha Camera, Processor, Chaji na Battery, Umbo na Muundo, Rom na Ram, Android, Display, Refresh rate na connectivity na kukupa majibu ipi ni bora zaidi kwa matumizi yako.

Camera

Kwanini Infinix Note 30 ni Simu Bora Kuliko Galaxy A24

Infinix kwa upande wa camera simu huwa na Camera mbele na nyuma Note 30 ina Megapixel 64+8+2 za Camera ya nyuma na Megapixel 16 za Selfie Camera, Samsung A24 Megapixel 50+5+2 za Camera ya nyuma na Megapixel 13 za Selfie Camera hivyo kwa mujibu na number of pixel NOTE 30 inatupa picha nzuri zaidi ukilinganisha na A24.

Advertisement

Processor

Chipset zinalingana simu zote mbili zinatumia Mediatek Helio G99 na CPU kwa simu zote mbili ni 2.2GHz Octa Core Processor hivyo tunaona Infinix NOTE 30 na A24 zina speed sawa katika kuipa nguvu simu wakati wa kuendesha applications mbalimbali kama vile kucheza games, kudownload, kuperuzi n.k.

Chaji na Battery

Kwanini Infinix Note 30 ni Simu Bora Kuliko Galaxy A24

Simu zote mbili zinatumia battery ya ujazo wa mAh 5000 isipokuwa tofauti inakuja kwenye fast chaji Infinix NOTE 30 ina Watt 33 na A24 ina Watt 25, kulingana na namba za Watt Infinix NOTE 30 inapitisha moto kwa haraka zaidi kufikia kwenye battery la simu na kuijza ndani ya muda mfupi na kulingana na majaribio inachukua nusu saa tu kwa Infinix note 30 kujaa chaji kwa 70%.

Umbo na Muundo

Ni zenye umbo tambarare na jemba, mbele zimetawaliwa na wigo mpana wa kioo, frame zake ni plastic isipokuwa nyumba zinatofautiana A24 jalada la nyumba ni plastic wakati Infinix NOTE 30 jalada la nyuma ni material ya Glass na leather. Muundo wa NOTE 30 ulijizolea Tuzo ya PARIS AWARD 2023 katika kipengele cha best product design/Media and Home Electronics.

Rom na Ram

Infinix Note 30 ina wigo mkubwa wa kuhifadhia kumbukumbu Rom yake ni hadi GB256 na Ram ni GB 8 na inaongezeka hadi kufikia GB16 wakati A24 ina Rom ya GB125 na Ram ya GB 6 hivyo basi ukubwa wa Rom na Speed ya Ram ya Infinix NOTE 30 ni mara mbili kwa A24.

Display na Refresh Rate

Kwanini Infinix Note 30 ni Simu Bora Kuliko Galaxy A24

A24 inakioo cha AMOLED na Infinix NOTE 30 ina kioo cha IPS kioo cha AMOLED ni bora katika kuleta rangi nzuri ya picha na IPS ni kizuri sababu hakivunjiki kwa wepesi hivyo kila kampuni ina namna yake yakutamba katika hili. Refresh rate inaongeza ubora katika kioo sababu refresh rate inapokuwa kubwa inafanya kioo kuwa smooth zaidi, Infinix NOTE 30 ina refresh rate 120Hz na A24 ni 90Hz.

Android na Connectivity

Kwanini Infinix Note 30 ni Simu Bora Kuliko Galaxy A24

Simu zote zinatumia Android mpya ambayo ni Android 13 kupitia simu hizi unapata applications ambazo ni latest na kwa upande wa Network zote ni 4G sababu tumelinganisha sifa ya Infinix NOTE 30 ya 4G na A24 ya 4G.

Sauti Speaker

Kwanini Infinix Note 30 ni Simu Bora Kuliko Galaxy A24

Infinix ina dual speaker lakini pia imeshirikiana na JBL katika kuhakikisha ubora wa sauti, Samsung ina speaker moja.

Upatikanaji

Zinapatikana katika maduka yote ya simu, vile vile Infinix NOTE 30 inapatikana kwa mkopo katika kipindi hiki cha promosheni ya JIPATE NA INFINIX @infinixmobiletz.

Tembelea page za katika mitandao ya kijamii kwa huduma ya haraka kwa unapenda wa Infinix unaweza wacheck kupitia namba 0659987284

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use