Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni

Unataka kumiliki biashara au kampuni mtandaoni, haya hapa mambo ya muhimu
Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni

Watu wengi hudhani kuwa kuanzisha kampuni au biashara mtandaoni ni lazima kuanza na hatua kubwa kama kuwa na ofisi kubwa, kuwa na wafanyakazi pamoja na vitu vingine vingi. Lakini leo napenda nikwambie kuwa unaweza kuanzisha kampuni kwa kutumia laptop au simu yako pamoja na internet tu, bila kuwa na ofisi wala kitu chochote.

Kupitia makala hii nitaenda kukupitisha kwenye hatua zote ambazo unaweza kufanya ili kuweza kuanzisha kampuni yako kupitia mtandao. Njia hizi ni njia ambazo binafsi nilipitia hadi kuweza kumiliki ofisi yenye uwezo wa kuhudumia wateja mbalimbali, kumbuka kitu cha msingi ni kuwa na nia ya kufanya kitu kwani kuna baadhi ya hatua huchukua muda mrefu na unaweza kukata tamaa kama wewe sio mvumilivu.

Basi najua hupendi maneno mengi hivyo moja kwa moja twende nikakupitishe kwenye hatua zote hadi ufanikiwe kuwa na kampuni yako.

Advertisement

Fungua Sanduku la Posta

Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni

Unakubaliana na mimi kuwa sio kila mtu analo sanduku la posta, lakini kila kampuni ambayo ina endana na wakati ni lazima iwe na sanduku la posta. Sanduku hilo linaweza kukusaidia kufanya mambo mengi sana kama vile kupokea barua pamoja na mambo mengine mengi ambayo ni muhimu kwa biashara yako. Kama upo Tanzania unaweza kutembelea tovuti ya posta ili kupata njia za kufungua sanduku la posta kirahisi la kidigitali kwa urahisi. Unaweza kufungua sanduku lako mwenyewe bila kuhudumiwa na mtu yoyote.

Fungua Sanduku la Posta Hapa

Sajili Jina la Biashara au Kampuni

Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni

Jina la biashara yako ni moja kati ya kitu cha muhimu sana, hapa ni vyema kuchagua jina bora na ambalo litakusaidia kukuwa kibiashara bila kuvunja sheria, bila kuwa na maana mbaya kwa wateja wako na ambalo pia ni rahisi kutamka na kukumbuka. Unaweza kusoma hapa ili kupata msaada wa kupata jina lako la biashara. Sasa baada ya kusema hayo basi naweza kukwambia kuwa kusajili jina la biashara ni rahisi na haraka na huna haja ya kwenda popote zaidi ya mtandaoni.

Sajili Jina la Biashara Hapa

Tengeneza Website ya Kampuni na Barua Pepe

Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni

Najua mpaka unafikia hatua hii basi umeshajua unahitaji kufanya kitu gani kwenye kampuni yako. Hivyo basi, hatua inayofuata ni ya muhimu ambayo ni kuanzisha tovuti au website kwa ajili ya kampuni yako. Hapa sasa unaweza kufuata njia hizi rahisi ambazo unaweza kufanikiwa kutengeneza website yako ya kampuni kwa gharama ya elfu 3000 tu. Hatua ya kwanza soma makala hii lakini hakikisha unasoma hapa ili kununua domain ya .COM kwa gharama ya Tsh 3000.

Jinsi ya Kutengeneza website ya Bure Hapa

Jinsi ya Kutengeneza Domain ya .COM kwa Tsh 3000

Sajili Biashara Kupitia Google Business na Zoom Tanzania

Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni

Kama wewe mmoja wa watu wenye lengo la kupata masoko kutoka hapa nchini Tanzania basi hatu inayotakiwa kufanya sasa ni kusajili biashara yako kwenye tovuti ya Google Business na kwenye tovuti ya Zoom Tanzania. Hii itakusaidia sana hasa kwenye masoko yako kwa hapa nchini. Ili kusajili akaunti kwenye Google Business unatakiwa kuwa na sanduku la posta hivyo ni muhimu kufuata hatua ya kwanza kwenye makala hii. Kumbuka kwa sasa unaweza kuchagua location ya mahali unapoishi na unaweza kubadilisha location baadae.

Sajili Kurasa ya Google Business Hapa

Jisajili Kupitia Zoom Tanzania Hapa

Tengeneza Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni

Kama bado hujafanya hatua hii basi hapa ndio mahali kwa muhimu kufanya hivyo, hakikisha unapata username kwenye mitandao ya kijamii, username ambayo inaendana na jina la kampuni yako. Hii itakusaidia sana hasa pale wateja wanapo tafuta jina la kampuni yako kwenye mitandao ya kijamii. Unaweza kutafuta username kwa kutumia njia hapo chini.

Angalia Username ya Akaunti yako Hapa

Tengeneza Namba Kwaajili ya Kampuni

Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni

Hatua hii ndio pekee ambayo unahitaji kufuatilia kwa kwenda mahali kwenye ofisi, lakini pia hatua hii ni rahisi na haraka. Moja kati ya kampuni ambayo inatoa namba za simu za kuchagua ni kampuni ya TTCL. Kupitia kampuni hii unaweza kupata namba ya simu ya kampuni ambayo inaweza ikawa msaada mkubwa kwako. Hakikisha uchanganyi namba ya kazi na namba ya kampuni kwani hii inaweza kuleta mchanganyo mkubwa wa mambo ya ofisi na mambo ya binafsi, jitahidi sana kuapata namba ya simu ambayo itakuwa maalum kwa kampuni yako.

Tangaza Biashara Yako Kupitia Instagram

Hatua za Awali za Kuanzisha Biashara Mtandaoni

Hapa nadhani unajua ni kwanini nakwambia ufanye promotion kupitia Instagram kwanza, hii ni muhimu kwa kuwa watumiaji wengi hapa Tanzania wanapenda kutumia mtandao wa Instagram hivyo ni rahisi kufikia wateja kwa urahisi sana. Unaweza kufanya hivi kwa urahisi kwa kufuata njia hapo chini. Pia unaweza kutangaza biashara yako kwenye mitandao mingine kama Facebook na mitandao mingine ya kijamii.

Jinsi ya Kutangaza Instagram kwa Kutumia M-Pesa Mastercard

Amini usi amini, njia hizi zinafanya kazi kwa asilimia 100, kitu cha muhimu hakikisha tayari umepata uhakika ni kitu gani unataka kufanya kabla ya kuanza hatua hizi. Pia hakikisha una fuata sheria zote za nchi ambazo zinaendana na aina ya biashara unayofanya, pia ni vyema kuchukua muda wako kutafiti aina ya biashara unayotaka kufanya kabla ya kuanza hatua hizi kwani pindi utakapo anza hatua hizi basi moja kwa moja wateja watanza kupokea kampuni yako kama sehemu muhimu kwenye maisha yako ya kila siku.

Natumaini njia hizi zinaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine, kama unataka kujua zaidi jinsi ya kuanza biashara mtandaoni unaweza kutembelea kipengele cha pesa mtandaoni ili kujifunza mambo mengi zaidi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use