Jinsi ya Kufuta Tweet Zako Zote Kupitia Mtandao wa Twitter

Kupitia njia hizi utaweza kufuta zaidi ya tweet 2000 kwa mara moja
Jinsi ya Kufuta Tweet Zako Zote Kupitia Mtandao wa Twitter Jinsi ya Kufuta Tweet Zako Zote Kupitia Mtandao wa Twitter
Image Credit: Humannet/Shutterstock

Kuna sababu mbalimbali za kufikiria kuanza upya kupitia akaunti yako ya mtandao wako wa Twitter, pamoja na sababu hizo ni vyema kufahamu kuwa Twitter haina sehemu maalum ambayo inaweza kusaidia kufuta tweet zako zote.

Kuliona hilo leo tumekuletea njia tatu ambazo unaweza kutumia kuweza kuanza kufuta tweet zako zote na kuanza upya kupitia akaunti yako ya Twitter. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye njia hizi.

Tweet Delete

Jinsi ya Kufuta Tweet Zako Zote Kupitia Mtandao wa Twitter

Advertisement

TweetDelete ni mojawapo ya huduma maarufu zaidi za kusaidia kufuta Tweets zako. Ukiwa na huduma hii, una chaguo la kufuta kwa wingi tweet na utaweza kufuta tweet zako kiotomatiki.

Kwenye akaunti isiyolipishwa au akaunti ya bure, TweetDelete inaweza kuondoa hadi tweet 3,200 bila kukuhitaji upakie kumbukumbu yako ya Twitter.

Iwapo ungependa kufuta zaidi ya tweet 3,200, itabidi upate toleo la kulipia, Kwa mtu yeyote aliye na chini ya tweets 3,200, TweetDelete huenda ikawa chaguo lako bora kwani ni rahisi sana kutumia.

Tembelea Tovuti Hapa

Tweet Eraser

Kama ilivyo kwa TweetDelete, TweetEraser hukuruhusu kufuta hadi tweets 3,200 bila malipo. Walakini, inashauriwa upakie kumbukumbu yako ya Twitter ili kufanya hivi, na kufanya TweetEraser kufanya kazi vizuri zaidi.

Unaweza kujifunza hapa jinsi ya kupata file la lenye kumbukumbu la ZIP kutoka mtandao wa twitter, file ambalo unaweza kutumia kwenye tovuti ya TweetEraser.

Baada ya kupata file lako lenye kumbukumbu ya Tweet zako zote moja kwa moja ingia kwenye tovuti hii na weka file lako ulilo pakua kwenye mtandao wa Twitter kama inavyo onekana hapo chini.

Jinsi ya Kufuta Tweet Zako Zote Kupitia Mtandao wa Twitter

Tembelea Tovuti Hapa

Tweet Deleter

Chaguo jingine la kuaminika ni TweetDeleter. Hili ni chaguo la kulipia ambalo litakuhitaji ulipe kila mwezi, lakini kabla ya kukataa chaguo hili moja kwa moja, kwanza tusikilize. TweetDeleter ina vipengee vya kupendeza ambavyo unaweza kuwa tayari kulipia.

Jinsi ya Kufuta Tweet Zako Zote Kupitia Mtandao wa Twitter

Toleo lisilolipishwa linatosha kufanya kazi ndogondogo za kuangalia tovuti hiyo inavyofanya kazi ila kama unataka tovuti hii iweze kukusaidia basi ni vyema kulipia.

Pia TweetDeleter ni rahisi kutumia hata kwa mtu asiyejua kutumia programu yoyote na pia inaweza kufanya kazi kwa haraka zaidi.

Tembelea Tovuti Hapa

Na hizo ndio njia bora ambazo unaweza kutumia kuanza upya kwenye mtandao wa Twitter, kumbuka njia ambayo Twitter wanashauri ni kufuta tweet moja baada ya nyingine lakini kama unazo tweet nyingi sana basi pengine ni vyema kuangalia njia nyingine kama hizo hapo juu.

Kama unataka kujua zaidi jinsi ya kufuta post zako zote kwenye mtandao wa Instagram basi endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuletea njia hii hivi karibuni.

Kuwa wa kwanza kupata habari zote mpya kwa haraka hakikisha unapakua app ya Tanzania Tech kupitia simu yako ya Android Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use