Popular Now
Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026 1

Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra 2

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini 3

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini

Facebook GIF

Facebook Yaleta Kibonyezo cha GIF Kwenye (Maoni) Comments

Katika kusherekea kuanzishwa kwa GIF au Graphics Interchange Format Facebook imeleta sehemu mpya ambayo nauhakika kwa namna moja ama nyingine tayari umesha iyona au kusikia kwenye programu ya WhatsApp.

Sehemu hii sasa inakuja kwenye sehemu ya maoni au comment ambapo sasa utaweza kubofya hapo na utaweza kuweka picha zenye kucheza ambazo utapewa na Facebook kupitia kwenye database yake ya GIF kama ilivyo kwenye whatsapp.

Kwa kutumia sehemu hiyo sasa uataweza kuacha maoni yako kwenye picha ya mtu kwa kutumia picha, hata hivyo Facebook inaonekana kujikita sana kwenye swala zima la kutumia GIF baada ya sehemu ya GIF kuja kwenye programu ya WhatsApp ambayo wote tunajua ni sehemu ya kampuni ya Facebook, labda tusubiri kidogo pengine sehemu hii itaweza kuja kwenye mtandao wa Instagram pia. Kujua jinsi ya kutumia sehemu hiyo angalia video hii….

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Previous Post
Judy Malware on Android

Kama Unatumia Simu ya Android Soma Hii ni Muhimu Sana

Next Post
facebook kupambana na magaidi

Facebook Kutumia (AI) Artificial Intelligence Kupambana na Ugaidi