Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

“Circle to Search” Sasa Inapatikana Kwenye Simu za Galaxy A

Kama unatumia Galaxy A55, A54 na A34 sasa unaweza kutumia sehemu mpya ya Circle to Search
"Circle to Search" Sasa Inapatikana Kwenye Simu za Galaxy A "Circle to Search" Sasa Inapatikana Kwenye Simu za Galaxy A

Kampuni Google kwa kushirikiana na Samsung hivi karibuni ilizindua sehemu mpya ya inayotumia AI ya Circle to Search kwenye Simu zake za Galaxy S24. Sehemu hii ina kuwezesha kutafuta “kusearch” kwa kuzungusha duara kwenye picha au sehemu ya picha unayotaka kutafuta.

Advertisement

Kwa mujibu wa taarifa mpya, sehemu hii ambayo awali ilikuwa inapatikana kwa watumiaji wa simu mpya za Galaxy S24 sasa inapatikana rasmi kwa watumiaji wa simu za Galaxy A Series.

Baadhi ya simu ambazo ni simu za awali kupata sehemu hii ni pamoja na simu za Samsung Galaxy A54, Galaxy A55, Galaxy A34 pamoja na Galaxy A35.

Kwa sasa bado hakuna taarifa kamili ni lini simu nyingine za Galaxy A Series zitapokea sehemu hii mpya ya Google, ila ni wazi kuwa simu nyingi za sasa za daraja la kati za Galaxy A Series ni lazima zitapokea sehemu hii mpya kutoka Google.

Sehemu hii ya Circle to Search, inaku wezesha kusearch kitu chochote kilichopo kwenye picha kwa urahisi na haraka. Sehemu hii ni bora zaidi hasa sasa ambapo mitandao ya kijamii inatumiwa zaidi na biashara pamoja na watu binafsi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use