Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Bill Gates Ajiunga na Instagram Mara ya Kwanza Akiwa Tanzania

Sasa tajiri namba moja duniani Bill Gates yupo kwenye Instagram
bill gates instagram bill gates instagram

Bill Gates tajiri namba moja duniani ni mmoja wa watu ambao walikua bado hawapo kwenye mitandao mingi ya kijamii ikiwepo instagram, hilo limebadilika jana baada ya tajiri huyo kujiunga na mtandao wa instagram kwa mara ya kwanza kabisa akiwa nchini Tanzania.

Bill Gates alijiunga na mtandao huo kwa jina la thisisbillgates, na kutuma picha ya kwanza iliyokuwa ikionyesha alivyoshiriki chakula cha mchana na watoto wa shule ya msingi ya kacheba na kukutana na watu mbalimbali ambao kwa mujibu wa post hiyo ya kwanza kutoka kwa bill gates alionekana kufurahishwa nao sana.

Advertisement

Hello from Tanzania, Instagram! I just had a great lunch with some amazing kids at Kicheba Primary School in Muheza and met Upendo Mwingira, a remarkable physician who has dedicated her career to fighting neglected tropical diseases. Melinda and I have been coming to Tanzania for many years now. I always love seeing how much progress the country has made to improve health and provide opportunity. Plus, the scenery is stunning. Whenever I travel to places like this, I wish others could come along and meet the people I get to meet. I have no doubt it would leave them as optimistic as I am about progress happening around the world. I’ll be sharing photos from my adventures here on Instagram, and I hope you’ll follow along.

A post shared by Bill Gates (@thisisbillgates) on


Mara baada ya kujiunga tu na mtandao wa instagram akaunti ya tajiri huyo ili hakikiwa na kupelekea follower wake kuongezeka kwa kasi sana na mpaka makala hii ina andikwa bill gates alikuwa na follower 25.2k.

Bill Gates kwa sasa ni tajiri namba moja duniani licha ya magazeti mbalimbali ya hapa Tanzania kuandika kuwa ni tajiri namba mbili, hii inatoka na tukio lililotokea mwishoni mwa mwezi ulio pita baada ya mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos kumpita Bill Gates kwa utajiri kwa kuongezeka kwa hisa zake kwa kasi, kitendo ambacho hakikudumu kwa muda mrefu na Hisa za Bill gates zilipanda tena na kumrudisha Bill Gates kuendelea kuongoza kuwa tajiri wa dunia.

Hata hivyo Bill Gates alikuja Tanzania hapo juzi na kulifikia huko muheza mkoani Tanga, akiwa katika kazi ya kuendeleza shirika lake lisilo la kiserekali la Bill and Melinda Gates Foundation ambapo baadae alikutana na Raisi wa Tanzania na kuongea mambo mbalimbali kabla ya Tajiri huyo kuondoka siku ya ijumaa jioni.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Forbes

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use