Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Tengeneza pesa mtandaoni kupitia soko la apps kama Play Store
Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Kama umekuwa nasi kwa muda mrefu basi unajua kuwa tumekuwa tukishirikiana kwa pamoja kuweza kuangalia njia za kusaidia vijana wenzetu kuweza kufanikiwa kwenye biashara mtandaoni.

Na siku ya leo tumekuletea njia mpya ya kuweza kuanzisha biashara yako inayo fanana na Google Play Store au soko la apps ambalo na uhakika linaweza kukusaidia kutengeneza pesa kwa urahisi kupitia Adsense au njia nyingine. Bila kupoteza muda twende moja kwa moja tuka angalie biashara hii.

Advertisement

Unahitaji Nini.?

Hapa ni muhimu kufahamu kuwa unahitaji mambo ya muhimu na kwa kuwa hapa utakwenda kutengeneza pesa kwa kutumia Adsense basi ni wasi kuwa unahitaji kuwa na tovuti au programu maalum.

Kwa kutumia njia hii, hapa unahitaji kuwa na tovuti na sio programu na ili kupata tovuti ni wazi unahitaji mambo matatu ya muhimu. Unahitaji kuwa na domain, unahitaji kuwa na hosting na pia unahitaji kuwa na akaunti ya Google kwaajili ya Adsense.

Kama unahitaji domain, tayari nilisha kuelekeza jinsi ya kupata domain ya Tsh 3000 kwenye makala hii, na kama unahitaji hosting basi unaweza kutumia hosting zile za bure kama sehemu ya majaribio, au unaweza kununua hosting ya bei nafuu ambayo unaweza kupata mtandaoni.

“Msingi ni muhimu kuliko kitu chochote, ukijenga msingi vibaya basi hata kile kinacho jengwa juu yake hakitaweza kudumu kwa muda mrefu.”

Tovuti kama Google Play Store

Miezi michache iliyopita tulitengeneza sehemu ya tovuti maalum ambayo itasaidia watanzania kuweza kutangaza app zao bila kulipia, hii ikiwa ni katika nia ya kusadia wabunifu wa kitanzania kufanikiwa zaidi na app zao kuweza kujulikana kwa haraka.

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Lakini sasa tovuti hii tumeifungua kama Open Source na hii ikiwa na maana kuwa mtu yoyote anaweza kumiliki tovuti hii kwa kufuata hatua hizi rahisi.

Sifa za Tovuti Hii

Ukweli ni kwamba biashara nyingi zinazolipa kwa sasa ni biashara za kusaidia watu au wafanya biashara wengine kufikia watu zaidi na tovuti hii inafanya hivyo kwa kiasi kikubwa.

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Kupitia tovuti hii huna haja ya kuweka apps hizi mwenyewe moja kwa moja bali ndani ya tovuti hii kuna mfumo maalum ambao utakusaidia kuweka app hizo kutoka kwenye soko la Play Store moja kwa moja kwenye website hii bila kupoteza muda mwingi.

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Kama unavyoweza kuona hapo juu, kupitia tovuti hii unaweza kutafuta app yoyote na moja kwa moja itaonekana kwenye tovuti hii na utaweza kuiweka kwenye tovuti hii kwa urahisi kwa kubofya sehemu ya Submit.

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Kwa kubofya submit, kila kitu kitaweza kuwekwa kwenye tovuti hiyo, ikiwa pamoja na screenshot icon ya app husika pamoja na maelezo ikiwa na link ya kupakua app hiyo moja kwa moja.

Hiyo ndio kazi pekee utakayokuwa unafanya yaani una search application pamoja na kuziweka kwenye tovuti hii moja kwa moja bila kufanya jambo la zaidi.

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Hivi ndivyo itakavyo kuwa pale ambapo utaweka app hiyo kwenye tovuti hii, na hapo moja kwa moja utaweza kuweka app mpya kila siku kwa urahisi.

Hakuna ukomo wa idadi ya apps ambazo unaweza kuweka, unaweza kuweka apps nyingi kadri utakavyo na moja kwa moja zitaweza kutokea kwenye tovuti hii kwa urahisi na haraka. Uzuri wa tovuti hii ni kuwa inakupa kurahisi sana wa kuweza kupewa matangazo na Google kupitia Adense.

Angalia Mfano wa Tovuti Hiyo Hapa (Haina Matangazo)

Angalia Mfano wa Tovuti Hiyo Hapa (Inayo Matangazo)

Matangazo ya Adsense

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Tovuti hii imetengenezwa kuhakikisha unapata kipato kikubwa kupitia Adsense na kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu sehemu za matangazo ni nyingi na zimetengenezwa kuhakikisha wewe unapata kipato kinacho faa kupitia Adsense.

Mpaka sasa tovuti hii inaweza kutengeneza hadi Dollar 7 kwa siku na kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo chini hayo ni mapato ya Adsense hadi jana tarehe 8/6/2020 muda wa saa tano asubuhi.

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Kwa mapato ya siku ya leo tarehe 9/6/2020 unaweza kuona hadi sasa saa tatu asubuhi tovuti hii imeweza kutengeneza kiasi gani kupitia picha hapo chini.

Jinsi ya Kuanzisha Biashara Mtandao Kama Play Store

Kama umekuwa ukipata shida ya kupewa matangazo na Adsense basi usijali kwani kwenye tovuti hii nina uhakika utapewa matangazo kwa asilimia 100 kitu cha msingi hakikisha unafuata vigezo na masharti ya Google ikiwa na njia bora za kupewa matangazo hasa hizi tulizo ziongea kwenye makala hii hapa, soma makala hiyo kujua zaidi.

Kumbuka : Matangazo ya Adsense yanaweza kuchukua hadi wiki mbili kuweza kuwashwa kwenye tovuti yako, pia unaweza kutumia muda wa hadi miezi miwili kuweza kupata pesa zaidi kupitia Google Adsense.

Unapateje Tovuti Hii.?

Sasa baada ya maongezi hayo marefu habu tuje kwenye upande wa bei, Unaweza kupata tovuti hii kwa bei mbili tofauti na zote zimeeleza kupitia hapa.

  • Tovuti Pekee – Tsh 100,000 Hapa utapata tovuti yenye uwezo wa kufanya kazi kwa asilimia 100 lakini itakuwa ni tovuti pekee. (Kumbuka gharama hizi hazihusiani na gharama za kununua domain, hosting au gharama nyingine zozote).
  • Tovuti Ikiwa Imekamilika na Domain na Hosting – Tsh 250,000 Hapa utapata website na utaweza kuunganisha vyote kwa pamoja na kuanza biashara yako kwa haraka. (Kumbuka hapa utapata website ikiwa imekamilika ikiwa pamoja na akaunti ya Google Adsense.).

Baada ya kulipa pamoja na kukubaliana unaweza kupata tovuti ndani ya siku moja (Ni muhimu kujua kuwa tovuti hii inaweza kubadilika rangi pamoja na logo vitu ambavyo unaweza kufanya mwenyewe kwa urahisi na haraka

Kwa watu 10 wa kwanza utaweza kupata tovuti hii kwa Tsh 110,000 ikiwa pamoja na domain pamoja Hosting ya mwaka mmoja bure na uta tengenezewa kila kitu na utaweza kupata tovuti hii ndani ya siku moja (Kutegemeana na Wingi wa watu) Wasiliana nasi hapa kama unataka tovuti hii au kama una maswali zaidi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use