Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apple Yatoa Toleo Jipya la iOS 11.2.2 (Muhimu Sana Ku-update)

Toleo hilo ni toleo linalo ongeza ulinzi juu ya virusi vya Spectre and Meltdown,
ios11.2.2 ios11.2.2

Hivi karibuni kampuni ya Apple imetoa Toleo jipya la iOS 11.2.2, toleo ambalo linategemewa kuweka ulinzi muhimu sana kwenye vifaa vya Apple vya iPhone, iPad pamoja na iPod.

Hata hivyo kampuni hiyo imesema kuwa ni muhimu kwa kila mteja kuangalia na ku-update kifaa chake kwenda kwenye toleo hilo jipya kwani linaongeza ulinzi juu ya aina mpya ya virusi vilivyo gunduliwa hivi karibuni.

Advertisement

Apple inasema kuwa vifaa ambavyo vina takiwa ku-update kwenye toleo hilo ni pamoja na vifaa vya iPhone kuanzia iPhone 5s na kuendelea, vifaa vya iPad kuanzia iPad Air na kuendelea pamoja na vifaa vya iPod kuanzia iPod touch 6th generation na kuendelea.

Hivi karibuni kumeibuka aina mpya ya virusi vinavyoitwa Spectre and Meltdown, virusi ambavyo viligundulikwa mapema mwaka huu kwenye vifaa vinavyotumia processor za intel. Hata hivyo asilimia kubwa ya kampuni zenye vifaa vyenye kutumia processor hizo kama Microsoft, Apple pamoja na Google tayari zimesha toa update mbalimbali ambazo zinalenga kuweka ulinzi juu ya virusi hivyo.

Kama unatumia vifaa vya Apple hasa iPhone, iPad na iPod ni vyema kuanza kuangalia update za kifaa chako kwani ni muhimu na zinaongeza ulinzi wa kifaa chako juu ya virusi huvyo vya Spectre and Meltdown. Ili ku-update, unganisha simu yako na internet kisha ingia kwenye Setting > General > Software Update, subiri kidogo simu itafute update hizo kisha utaona update hizo alafu download na install kwenye kifaa chako.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

5 comments
    1. Ingia kwenye Setting kisha bofya General kisha bofya Software update kisha subiri utaona update hizo kisha bofya download and install.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use