in

Vifaa Vyote Smartphone, Kompyuta, Tablet Viko Hatarini Kudukuliwa

Inawezekana tayari PC, laptop, tablet, au smartphone yako imesha-adhiriwa

Vifaa Vyote Smartphone, Kompyuta, Tablet Viko Hatarini Kudukuliwa

Hivi karibuni habari zimesamba mtandaoni na kuzua tafarani kuhusu uwezekano wa kudukuliwa kwa vifaa vyote vya kieletroniki vya smartphone, tablet na kompyuta za aina zote. Habari hizi zinakuja baada ya kugundulika kwa aina mpya ya virusi vya udukuwaji vilivyo gunduliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Google hapo mwaka jana.

Virusi vya udukuwaji huo ambavyo vimepewa jina la ‘Meltdown’ and ‘Spectre’ vinahusisha vifaa vyote vyenye kutumia processor za Intel, AMD pamoja na ARM na kwa upana wake asilimia kubwa ya vifaa vingi vya kielektroniki PC, laptop, tablet, na smartphone vinatumia processor za aina hizi.

Taarifa kutoka kwenye mitandao mbambali zinasema kuwa kupitia aina hiyo ya udukuaji, mdukuaji anaweza kutumia virusi hivyo kuchukua au kusoma vitu kama password, namba za siri za akaunti za bank za mtandaoni, kufungua programu mbalimbali kwenye kifaa chako pamoja na data zingine binafsi zinazopatikana kwenye vifaa vya PC, laptop, tablet, na smartphone zinazotumia processor za aina hiyo.

Kwa sasa haijajulikana ni dalili gani za kuangalia kama kifaa chako kimeadhiriwa lakini kampuni mbalimbali za kielektroniki kama za Apple na Microsoft zinasema kuwa kwa sasa wateja wake ni vyema kuchukulia kuwa ni vifaa vyote vimeadhiriwa au vinaweza kuadhiriwa.

Hivi leo kampuni ya Apple imetoa ripoti kuwa uwezekano wa vifaa vyote vya Apple kuadhiriwa na udukuaji huu ni mkubwa sana na tayari kampuni hiyo imesha-anza vita vya kupambana na virusi hivyo vya ‘Meltdown’ and ‘Spectre’ kwa kuandaa matoleo mapya ya mifumo ya uendeshaji ya vifaa vyake vya Mac, iPhone na iPad. Kwa upande wa Microsoft tayari imesha-anza kutoa update za Windows ambazo zilianza kutoka rasmi kuanzia siku ya jumatano.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya businessinsider baadhi ya vifaa vya zamani vinavyotumia mifumo ya Windows vitadhiriwa zaidi hata baada ya ku-install update hizo. Tovuti hiyo inasema kuwa vifaa hivyo vitapungua uwezo wake wa kufanya kazi kwa asilimia 5 mpaka asilimia 30. Hata hivyo vifaa vyenye processor za Intel’s “Skylake” vinasemekana kutoadhiriwa na update hizo.

Kwa sasa taarifa zinasema kuwa wateja wa vifaa hivyo hawana uwezo wowote wa kuzuia udukuaji huu zaidi ya kuhakikisha kuwa una update mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako, iwe unatumia Linux, Android, Apple’s MacOS, au Microsoft’s Windows 10 hakikisha una install update hizo ambazo zimesha anza kutokewa. Hata hivyo kwa mujibu wa Google udukuaji huu uwezeka kufanyika baada tu ya kuistall programu yenye virusi hivyo, hivyo basi ni vyema kuwa makini na programu mbalimbali unazo download na ku-install kwenye kifaa chako.

Kwa habari zaidi kuhusu virusi hivi vya Meltdown’ and ‘Spectre unaweza kusoma ukurasa maalumu wa meltdownattack.com pia endelea kutembea Tanzania tech tutakuwa tuki kuhabarisha muendelezo wa habari hii.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Hizi Hapa Movie Nzuri za Kuangalia Jumapili #1

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.