Apple Kuweka Application ya SIRI kwenye Mac Laptop

Apple Kuweka Application ya SIRI kwenye Mac Laptop Apple Kuweka Application ya SIRI kwenye Mac Laptop

Application maarufu katika simu za Apple kwa jina la SIRI inatarajiwa kuwekwa kwenye laptop za MAC za kampuni ya Apple, hayo yaliandikwa na blog maarufu ya habari za apple ya 9to5Mac. Kampuni ya apple kwa sasa inaandaa application hiyo kwaajili ya computer zake zote za apple, hata hivyo application hiyo inapatikana kwa sasa kwenye iPhone, iPad, iPod touch, Apple Watch, na Apple TV.

Ripoti zainasema kampuni ya Cupertino-based company itafanya uzinduzi rasmi wa application hiyo siku za karibuni karibia na mwezi june mwaka huu 2016 kwenye tamasha lijulikanalo kama “Worldwide Developers Conference”.

Blog ya 9to5Mac inaendelea kuandika kuwa Apple ilikua ikifanyia majaribio application hiyo kwa upande wa MAC computer toka mwaka 2012, hivi karibuni kampuni hiyo ndio imefanikiwa kutengeneza application hiyo inayoweza kutumika katika Computer za MAC. Kwa upande wa Microsoft kwa sasa na yenyewe inayo application inayofanya kazi kama SIRI ya Apple, application hiyo inajulikana kwa jina la “Cortana” application hiyo ilianza kutumika mwishoni mwa mwaka jana kwenye Operation System ya Windows 10.

Advertisement

Taarifa kutoka sehemu mbalimbali zinasema kuwa application hiyo itapatikana kwenye “Menu Bar” karibia na saa pamoja na Icon za Spotlight, pale mtumiaji anapo bonyeza kitufe hicho cha application hiyo ataletewa kama mfano wa mawimbi ya sauti ambapo itampasa mtumaji kuuliza chochote anachotaka kupitia application hiyo ya Siri ya computer za MAC. Taarifa zinaendelea kusema kuwa pale Computer ya MAC itakapochomekwa kwenye umeme mtumiaji atakua na uwezo wa kuiwasha application hiyo kwa kusema maneno “Hey SIRI”.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use