Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apple Kuleta Matoleo Mapya ya Laptop za Mackbook Mwaka Huu

Apple Kuleta Matoleo Mapya ya Laptop za Mackbook Mwaka Huu Apple Kuleta Matoleo Mapya ya Laptop za Mackbook Mwaka Huu

Kampuni ya apple imepanga kuboresha laptop zake za Macbook kwa kuleta matolea mapya ya laptop zake hizo kwa mojibu wa ripoti kutoka kwenye kampuni ya Cupertino Apple imepanga kuzindua laptop hizo kati ya mwezi April au June ripoti hizo ziliendelea kusema kampuni hiyo itatoa matoleo yake mapya ya 13-inch na 15-inch MacBook.

Hata hivyo kwa mojibu wa ripoti kutoka DigiTimes zinasema 13-inch na 15-inch MacBook laptop zitakua na muonekano unaofanana na ule wa Macbook ya 12-inch ambayo ilizinduliwa mwaka jana. Habari zinaendelea kusema kuwa laptop hizo mpya zitakua ni nyembamba zaidi ya zile za Macbook Air ambazo zipo sokoni kwa sasa pia zitakuwa na tundu moja la USB-C Port kama toleo la nyuma la Macbook ya inch 12, hata hivyo repoti hizo zilendelea kusema kua kampuni nyingine za laptop kama  Asus, Dell, na Lenovo pia zitatoa matoleo yake mapya ya laptop kipindi hichohicho.

Advertisement

Bado haija julikana kama Apple imepanga kutoa matoleo mapya kwenye laptop zake za MacBook Air na MacBook Pro ila repoti za awali zinasema Apple itatoa matoleo mapya ya Laptop zake zote ikiwa ni pamoja na MacBook, MacBook Air, MacBook Pro, Mac Pro, iMac na Mac Mini uzinduzi huo utafanyika mwaka huu kwa mojibu wa ripoti hizo.

Matoleo hayo mapya yamepangwa kuwa na processor ya  Skylake’ Core processor, Apple hawana kifaa chochocha notebook kinachotumia Processor ya Skylake’ Core processor. Hii inaonyesha vifaa hivyo vipya vitakuja na nguvu maradufu pamoja na muonekano mzuri.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use